Msaada wa mawazo kuhusu biashara ya viatu vya kimasai

kevoo 27

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
400
379
Habari wana jamvi,

Mimi nahitaji msaada wa mawazo kutoka kwenu juu ya biashara ya viatu vya kimasai au culture.

Mtaji wangu ni laki 5 ujuzi wa kutengeneza viatu vya kimasai ninao pamoja na cherehani sijawahi kufanya biashara hii ila huwa naona tu watu wanauza viatu hivyo mtaani na kwenye social media mbalimbali.

Nahitaji ushauri juu ya vitu vifuatavyo:
Soko lake likoje kwa ujumla?

Bei ya msasa au Mota ya 0.5 hp?

Na vitu gani vya kuzingatia kwenye biashara hii?
Mm Niko mwanza
Natanguliza shukrani zangu kwenu
Kwa wenye uelewa juu ya biashara hii naombeni mawazo yenu.
 
Ninajua in and out ya biashara hii! Zamani nilitengeneza mwenyewe na kusafirisha kuuza nje, pia niliuza online hasa Europe! sasa sijui malengo yako ni yapi hasa, utengeneze Tu then uwauzie watu hapa kwa jumla? Au utengeneze uuze mwenyewe!!
 
Lengo langu ni kuanzisha uzalishaji Mimi mwenyewe alafu kwa upande wa soko popote naweza kufika mladi tu uhitaji wa bidhaa hiyo uwepo.
Mm simple survey yangu nimetembelea maeneo kama katoro mkoani geita, kasuru mpaka kigoma mjini na kagera yote.
 
Mkuu hiyo cherehani ulinunua bei gani au wajua thamani ya hiyo cherehani
Hii cherehani kaka kiukweli bei yake cjui maana alinunua mzee kipindi cha nyuma maana kuna sister wangu alikuwa na garment sasa cherehani zipo tu home za umeme naza kawaida na hii ya viatu pia ipo.
 
Kwanza kama umeamua kuwa Mzarishaji mwenyewe, lazima productivity yako kwa siku iwe ya kutosha Sana, ili uweze kupata faida na kusema naacha vyote na sasa hii ndo kazi,binafsi sikuwahi kufikilia soko la Bongo coz lingenikatisha tamaa, niliamua kutafuta soko la nje ya Tanzania hasa zile nchi ambazo pesa zao zipo juu! Sikuwahi kupata hii nafasi uloipata wewe toka kwa mtu mwenye uzoefu!

Binafsi nilikua sipeleki hizo Masai Sendo pekee, nilikua nachanganya na kazi zingine za Sanaa ambazo zote niliandaa mwenyewe! Sasa ntaongelea soko la nje coz ndo nna uzoefu nalo.

Soko langu kubwa ambalo nilikua napeleka mzigo mwenyewe ukiacha kuuza online, lilikua Cape town South Africa, Kuna sehemu wanaita Market ni town center, kwenye Curio shops za Sanaa, kubwa na ndogo, pia nilikua napeleka sehemu wanaita Sea view, pia Kwenye Sunday Market mbalimbali hapo Cape town, Johannesburg nilikua napeleka sehemu moja wanapaita Rosebank, hapo mpaka Wabongo utawakuta!

Zambia nilikua napeleka Victoria false pia nilikua napeleka Botswana!

Hii ni biashara ya kazi ya Sanaa, na biashara ya Sanaa Africa yote Ina msimu mmoja, na Wateja wakubwa ni Wazungu wanaokuja kutalii, msimu huanza mwezi wa 6 mpaka wa 3 mwaka unaofata, so hapo Kati utafanya biashara popote Africa.

Ukipenda utauza jumla ukipenda rejareja, Masoko ni mengi Sana, ukiweza beba na Nguo za Masai, Batik ambapo sasa zina soko zuri Lesotho na nchi za kusini!

Uzuri wa biashara hii unafanya kwenye zile nchi ambazo pesa Yao Ina thamani, so utauza mzigo ambapo kwao wataona ni Cheaper, ilhari wewe ukija Ku change pesa Yao Bongo inakulipa zaidi!
 
Changamoto ambayo naiona kwako ni uzarishaji ili kuendana na soko, tuseme kama utafuma mwenyewe Shanga, kuunganisha kwenye Ngozi na kila kitu, lets say utaweza kutengeneza pair 2 tu kwa siku, kibongo itakua haikulipi coz utauza jumla, labda uajiri watu, kwa maana uwe na watu lets say 5 wanaosuka Shanga tu! 2 wanaokata Ngozi, mmoja kuunga Ngozi na Soli na mmoja kwa Cherehani, at least unaweza kukimbizana na Soko na ukapata faida.

Changamoto nyingine ni Ubunifu wa style na Ubora, ukiona Sendo style mpya mtaani na wewe ndo ukakimbilia kutengeneza! Itakula kwako sokoni, lazima uwe mbunifu, ujue namba ya Ku mix rangi za shanga n.k, ili utaposhusha mzigo tuseme Cape town, Sendo zionekane zina style tofauti na zina Quality, coz Kuna ushindani na Wakenya! Ila uzuri Wakenya wana copy kwetu then wanafanya kimtindo wao! So bado tupo juu kwenye ubunifu!

ni hayo Tu! But kama Una swali karibu.
 
Nashukuru sana kaka kwani umenipa njia wapi pakuanzia!

Na mawazo yako nimeyachukua kama yalivyo nitayafanyia kazi.

Ila Kuhusu Swala la ubunifu nipo vizuri kiasi flani maana kwa sasa nashona bracelets au culture kwa kutumia Shanga na beads (zile Shanga kubwa kubwa) za mkononi

Vipi Kuhusu msasa unaweza unapatikana kwa bei gani?
 
Msasa Mita 1. ni 3,000 kama sikosei, kwa size yoyote, pia wanauza nusu na robo mita!
 
Changamoto ambayo naiona kwako ni uzarishaji ili kuendana na soko, tuseme kama utafuma mwenyewe Shanga, kuunganisha kwenye Ngozi na kila kitu, lets say utaweza kutengeneza pair 2 tu kwa siku, kibongo itakua haikulipi coz utauza jumla, labda uajiri watu, kwa maana uwe na watu lets say 5 wanaosuka Shanga tu! 2 wanaokata Ngozi, mmoja kuunga Ngozi na Soli na mmoja kwa Cherehani, at least unaweza kukimbizana na Soko na ukapata faida.

Changamoto nyingine ni Ubunifu wa style na Ubora, ukiona Sendo style mpya mtaani na wewe ndo ukakimbilia kutengeneza! Itakula kwako sokoni, lazima uwe mbunifu, ujue namba ya Ku mix rangi za shanga n.k, ili utaposhusha mzigo tuseme Cape town, Sendo zionekane zina style tofauti na zina Quality, coz Kuna ushindani na Wakenya! Ila uzuri Wakenya wana copy kwetu then wanafanya kimtindo wao! So bado tupo juu kwenye ubunifu!

ni hayo Tu! But kama Una swali karibu.
kweli kabisa ndugu ubunifuu ndio kila kitu katika hii biashara mimi mwenyewe ninatengeneza ila siweki shanga na watu wanavipenda kitu cha msingi ni kutengeneza kwa stail ya kwako tu usiige kwa watu wengine coz vitafanana na ndio maana dar vimeshuka bei kwa sababu viatu vingi vinafanana kama vimetengenezwa na mtu mmoja, nikiongeza mtaji nitakutafuta ndugu unipe dondoo za kupeleka mzigo huko bondeni.
 
Sure Mkuu! Usijari karibu Sana!
 
Baada ya kimya kirefu hatimae nashukuru Mungu uzalishaji umeanza,
Ahsateni sana kwa mchango wa mawazo wa jf wote , tuzidi kushauriana na kkupeana channels
IMG_20170727_090619.jpg
IMG_20170727_090519.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kimya kirefu hatimae nashukuru Mungu uzalishaji umeanza,
Ahsateni sana kwa mchango wa mawazo wa jf wote , tuzidi kushauriana na kkupeana channels View attachment 551701View attachment 551702

Sent using Jamii Forums mobile app
Ongera Sana ndugu.
Naomba kukuuliza kutokana na experience yako kwan nami nna ndoto ya biashara hii
1.bado unaendelea na biashara hi?
2.vipi ukuaji wa soko ukoje?
3.Soko lako kubwa liko wapi kwa Sasa?
4.unauza jumla au rejareja
5.natakiwa kuandaa shilingi ngapi angalau kuanza?
 
kweli kabisa ndugu ubunifuu ndio kila kitu katika hii biashara mimi mwenyewe ninatengeneza ila siweki shanga na watu wanavipenda kitu cha msingi ni kutengeneza kwa stail ya kwako tu usiige kwa watu wengine coz vitafanana na ndio maana dar vimeshuka bei kwa sababu viatu vingi vinafanana kama vimetengenezwa na mtu mmoja, nikiongeza mtaji nitakutafuta ndugu unipe dondoo za kupeleka mzigo huko bondeni.
Mkuu Bado unafanya
SHUHULI hi?
 
Back
Top Bottom