Msaada wa mawazo katika hili

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,926
2,777
Wadau,

Kuna mdogo wangu amesomea kada ya biashara katika elimu yake ya upili (O-Level) na kwa sasa anafanya shahada ya Ugavi (Degree of Procurement and Supply) kwenye chuo kimoja maaraufu hapa jiji DSM.

Sasa amekata shauri anataka kusomea Nursing lakini O-Level alifanya mchepuo wa biashara akiwa amefanya Biology tu kama somo la lazima na Alipata daraja E kwenye somo ilo.

Anataka kure-seat masomo mawili ya O-level kwa maana ya somo la Phisikia na kemia haya ni masomo ambayo hakufanya kabisa kwa vile yapo kwenye mchepuo wa sayansi. Je inawezakana akafanya kama re-seater akitumia namba yake ya O-Level bila kipingamizi kutoka baraza la Mitihani (NECTA).

Lengo lake ni kuanzia level ya cheti katika kada ya NURSING bila kujali elimu aliyonayo kwa maana ya cheti na diploma ya procurement and supply.

Je nimaamuzi sahihi kwake kwa sasa?
 
Hujasema ni kwa nini amekata shauri?

Lakini kama ni kwakua anapenda kusomea masomo hayo (Nursing) Mimi sioni tatizo maana anakwenda kukamilisha ndoto zake.

Na raha ya kusoma usomee unachokipenda.

Na kuhusu uwezekano wa jambo hilo, ngoja tuwasubiri wajuzi waje kutufahamisha.
 
Back
Top Bottom