Msaada wa Kuunganisha PDA na internet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa Kuunganisha PDA na internet

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Ozzie, Jan 4, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nina PDA aina ya ASUS mypal A626 ambayo haina sehemu ya kupachika SIM card. Kwa sasa ninaweza nikaitumia sehemu yoyote penye Wi-Fi au Wireless network yeyote ile. Ningependa niitumie kwa internet ya kampuni za simu za mkononi kama Zantel au Vodacom kama tufanyavyo kwa simu za mkononi. Nijuavyo mimi kuna namna kampuni ya simu husika yaweza kuipa namba bila SIM card kama baadhi ya modem za Zantel ambazo huwa zinapewa namba bila kuweka SIM card. Maana nilipita nayo kwenye Voda na Zantel shops za mkoa mmojawapo pembezoni mwa nchi yetu wakaniambia labda Voda au Zantel makao makuu wanaweza kunisaidia. Hivi yawezekana kwa Tanzania?
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hiyo PDA haina uweza wa kuunganishwa na Internet ya kampuni ya simu. Haina radio ya simu, ni Wifi tu.
  Labda kuna uwezekano wa kutumia simu kupata net, then kuunganisha simu na hiyo PDA through Bluetooth au Wifi na kushare connection.
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hivi wifi ni nini wajameni, maana nina simu yangu kimeo HTC MDA vario II imekufa radio baada ya kuiangusha, radio chip ikawa dameged,no calls no sms no internet through sim card.
  lakini naambiwa naweza kupata internet kwa wifi, natamani nijaribu sikumoja nione, niwapi naweza enda nikapata hayo mawasiliano ya wifi,nimedokezwa eti naweza pata ktk migahawa ya steers.
  sorry kama nipo nje ya mada
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Wifi ni hizi Wireless internet za nyumbani au za ofisini ambazo laptop kwa kawaida huwa zinaconnect. Sijui kama Steers wana free Wifi.
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nashukuru mkuu, ila engineer wa Zantel kaniambia inawezekana hivyo niipeleke.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Mtakuwa hamjaelewana, nikiangalia specs za hiyo PDA sioni uwezekano wa kuunga na net, haina required hardware.
   
Loading...