Samahani wadau nilikua naandaa matokeo ya wanafunzi wetu hapa shuleni sasa kwa kutumia excel nimeshndwa fomular za kuweka last top 10.
Hivyo kwa anayefahamu anisaidie tafadhali
Kwenye ranking umetumia category gani? Eg average, division etc
Kama column ya ku-rank (column inayoonesha position za wanafunzi) ipo mbele ya column ya majina, itakubidi utumie reverse lookup, kama utashindwa insert column ya rank kabla ya column ya majina ili utumie lookup function ya kawaida.
Tengeneza table yenye column mbili (C50
😀59), column moja ipe jina S/N (1 mpaka 10 tufanye ni column C) na nyingine ipe jina STUDENT NAME (tufanye ni column D). Juu ya table unaweza ukaandika title BOTTOM TEN STUDENTS
Katika column D tumia hii formula, then scroll mpaka D59
=Vlookup(Large(C50,$B$5:$B$45),$B$5:$H$45,2,FALSE)
Where
Column B ni column ya rank/position (hiyo B5:B45 ni mfano, wewe utaanzia inapoanza table yako mpaka inapoishia eg B15:B250)
B5:H45 ni table yako uliyotumia kujaza hizo details zako, pia ni mfano. Utaangalia table yako imeanzia wapi na kuishia wapi eg D10:J250 etc
Note: Hiyo formula utaitumia endapo column ya rank na column ya majina zimefatana (ambapo inatakiwa ianze column ya rank, vinginevyo hapo kwenye 2 haitokuwa mbili tena itakuwa 3,4 etc)