Msaada wa kulipwa gari

prakatatumba

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
1,333
1,250
Habari zenu wana JF!wiki iliyopita nilipata ajali maeneo ya Tabata, sasa tulienda police tukafungua jalada na likapelekwa mahakamani. Nina hitaji kulipwa kutoka insurance ila nimeambiwa natakiwa kupeleka claim form, mchoro, pf 90 na 93.

sasa tatizo linakuja hapa;
1. insurance wananiambia hizo doc zinapatikana na hazihitaji kusubiri mambo ya mahakama na
2. police wananiambia hizo doc mpaka jalada la kesi lirudi kutoka mahakamani.

Wenye uelewa au uzoefu wa hizi taratibu naomba nipate ukweli na nifanye nini wadau. Natanguliza shukrani zangu za dhati
 
Mu-sir

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,624
2,000
Penye udhia penyeza rupia. Kama umeelewa hapo mambo yatakuendea haraka
 
jubilant

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
308
500
Habari zenu wana JF!wiki iliyopita nilipata ajali maeneo ya Tabata, sasa tulienda police tukafungua jalada na likapelekwa mahakamani. Nina hitaji kulipwa kutoka insurance ila nimeambiwa natakiwa kupeleka claim form, mchoro, pf 90 na 93.

sasa tatizo linakuja hapa;
1. insurance wananiambia hizo doc zinapatikana na hazihitaji kusubiri mambo ya mahakama na
2. police wananiambia hizo doc mpaka jalada la kesi lirudi kutoka mahakamani.

Wenye uelewa au uzoefu wa hizi taratibu naomba nipate ukweli na nifanye nini wadau. Natanguliza shukrani zangu za dhati

Sio Kweli hata kidogo
utaratibu ni

1. Uwe na inspection report ya police included michoro
2.Hii report utaipeleka kwa bima broker wako atakupatia claim form
3. Claim form utaipeleke polisi wao watakupatia pf 90 umemaliza

Hakuna swala la kusubiri mahakama, wewe unachoshindwa kuelewa, mshahara wa 180,000 wanaolipwa polisi hautoshi kuendesha maisha...Wahenga walisema "PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA."
 
kyemo

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
350
500
Mkuu ni hivi:
Ukipata ajali, unapewa mchoro,PF 90 na PF 93
Jalada kwenda mahakamani inategemea kama umegonga kitu au mtu lakini kama umepata ajali ya own damage/yani hujagonga kitu au mtu haiitaji kwenda mahakamani,hii pia inausisha na claim form.
Yani claim form inahitajika kama umegonga kitu au mtu kwa ajili ya yule mtu kwenda kupeleka madai kwenye bima yako na hapo ni lazima kesi iende mahakamani kwa ajili ya kuhukumiwa.

Kwa hiyo hapo mkuu akili kichwani mwako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom