Msaada wa kulinda Ajira hizi Tanzania

Msaada wa kulinda Ajira hizi Tanzania

Joined
Mar 24, 2017
Posts
6
Reaction score
2
Habari, Mheshimiwa Rais,Waziri Mkuu & waziri wa Mawasiliano/Waziri wa ajira & Maendeleo ya Vijana

1. Sisi ni sehemu ya wajasiliamali tuliopata ajila zetu ambazo sio rasmi kwenye mitandao ya simu (Freelancer)

Tulikuwa tunaomba msaada wako/ Wenu kutusaidia kurekebisha sheria mpya ya TCRA

Tumeambia kuwa kuanzia Trh 01/05 mwaka huu haitaruhusiwa mawakala wa usajili yaani (Freelancer's) kusajili line kwa kutembea mitaani kama Machinga!

Inatakiwa kila msajili line akodi Frem ya Biashara akate leseni pia awe na TIN na pamoja na Kitambulisho cha NIDA

Mfumo huu kwa mazingira ya nchi yetu hautakuwa rafiki kwa vijana wa kitanzania ambao wamepata ajila zao kupitia hii kazi,kwa vile wengi watashindwa kukodi milango na kukidhi vigezo vya kuwa wasajili kwa mfumo mpya

Kwa kushindwa kwao ina maana hawatakuwa na ajira tena

Lakini pili kwa kufungua milango ya biashara itafanya malipo yao yashuke sana kwa vile hawatapata wateja wa kutosha, Ikumbukwe kuwa kazi yetu hatulipwi mshahara bali tunalipwa Commission kwa kadri ya ufanyaji wa kazi, hivyo kwa mfumo wa kutembea inatulipa zaidi kuliko kuwa (fixed) sehemu moja.

Nini mawazo yetu!

Kama lengo ni kulipa kodi tunaunga mkono Serikali yetu kwa vile kweli hii kazi inatupa kipato cha kutosha na hasa wengi wetu, Hatuwezi kuajirika katika soko la ajira kwa vile Elimu zetu ni za chini! Lakini tunashukuru sana makampuni ya simu yametupa ajira Vijana wa Kitanzania zaidi ya Elfu 50 kwa vigezo vya kujua kusoma na kuandika pia uwezo wa kuelezea bidhaa za makapuni kwa wateja wetu! Kwa hiyo tunaunga mkono kulipa kodi kwa vile tunapata kipato. Hivyo, kulipa kodi sio shida hata kidogo tunatambua Serikali lazima ijiendeshe kwa sisi Raia kulipa kodi sitahiki

Pendekezo letu tunaomba kwa vile Commission zetu tunalipwa kila mwezi serikali iweke sheria kwa sisi ambao tupo kwenye mitandao ya simu na tunalipwa kwa Commission tukatwe kodi moja kwa moja tunapolipwa Commission zetu, Mfn kama sheria ikisema tulipe asilimia kumi ya Commission zetu kila mwezi tunaweza kulipa kodi kubwa sana kuliko tukifungua frem ambazo ni fixed!

Kwa taarifa tulizonazo Kampuni zote za simu wanalipa Commission zaidi ya Bilioni 6 kila mwezi kwa vijana hawa wanaosajili line kulingana na makubaliano na Makampuni yao

Kwa mfano piga hesabu ya kukata 10% ya Bilioni 6,utaona jinsi Serikali itapata kodi kubwa kwa mwezi/mwaka, na kodi ambayo haitasumbuka kuipata kwa vile atapata kupitia moja kwa moja kwa makapuni kama serikali inavyopata kodi za wafanyakazi wengine kupitia waajili wao

Pendekezo lingine kama tatizo ni kupunguza uharifu serikali na makampuni ya simu wana wataalamu wazuri wa IT wanaweza kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti vijana wasisajili line na kuwauzia watu ambao ni waharifu tunaimaini kuwadhibiti watu wachache ambao sio waaminifu inawezekana kuliko kuua ajira za Mamilioni ya Vijana kwa sababu ya watu wachache.

Mfn inaweza kuweka System mteja akisajili line moja apate taarifa kwenye namba anazomiliki mteja huyo kuwa amesajili line ya mtandao X,hivyo mteja atajua kuna line imesajiliwa na Msajili hajampa,au Mteja akatumiwa Password(OTP) kwenye line aliyonayo kwa hiyo ili line isajiliwe lazima mteja atoe password hizo kwa Msajili, au ukisajili line moja uwekwe mda wa hata masaa 10 au siku 2 ndipo system iweze kukubali kupitisha line nyingine ya huyo mteja

Hii ni mfn tu ya njia za kudhibiti uharifu wa kusema rudia kuweka kidole System inasumbua

Lakini pia tukumbuke pia hizi pesa Bilioni 6 ambazo Makampuni ya simu wanazolipa vijana wa Kitanzania kama Commission zinaingia kwenye Mzunguko wa Uchumi wetu kila mwezi,japo hata sasa Serikali haipati kodi ya moja kwa moja ila inapata kodi kupitia bidhaa wanazonunua vijana baada ya kulipwa, lakini pia Mzigo wote wa hawa Vijana tukiwatoa kuanzia trh 01/05 Mwaka huu ni Ipi plan B ya Serikali itawasaidia?

Tunaomba Waziri wa kazi kwa kushirikiana na Waziri wa Mawasiliano mliangalie hili! Pia Ombi letu Waziri wa Mawasiliano Na Waziri wa kazi wapate mda waonane na sisi wajasiliamali tunaofanya hii kazi, sio tu kukutana na wenye makampuni ya simu bila kutusikiliza sisi ambao tunafanya kazi hii huku chini!
 
Acheni ujinga nyie. Kila mkisajiri namba moja mnasajiri na nyingine feki kwa tamaa zenu.

Kibano ni kuwa ukiwa na TIN, NIDA utatambulika, na ukisajili manyoka nyoka unafungiwa na kamisheni hupati.

CCM ni ile ile.
 
Ni kweli kiongozi hiyo changa moto kama wasajili tunaijua ipo,lkn kwa wengi wa sisi vijana ni waaminifu sana,ndio maana kama umesoma vzr hapo tumetoa na njia ya kudhibiti tatizo hilo kwa njia ya system!

Lkn ukichosema ni kweli changamoto hiyo ipo lkn sio tatizo kubwa kulinganisha na manufaa ya kupoteza ajira za vijana wote

Ni kama tu nyumba yako inaviroboto hutachoma nyumba ili unagamize viroboto utachukua njia nziri kuangamiza viroboto ukiacha nyumba ikiwa salama
 
Safi sana mkuu nafikiri TCRA wamekusikia na watalifanyia kazi. Ndo maana mama Samia aliwatukana TRA juzi wanafanya kazi kwa nguvu hawatumii akili na maarifa.
 
Back
Top Bottom