Msaada wa Kujikwamua

Msaada wa Kujikwamua

Abby The Rider

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
473
Reaction score
781
Habar wanajamvi

Natumai ni wazima na buheri wa afya. Niende kweny mada husika.
Nina msichana ambaye Niko nae kweny mahusiano kwa zaid mwaka na nusu sasa, kiufupi ni kwamba bado Niko nae na ananiheshimu na kunithamin sana japo hali ndo hio ya Jiwe..
Kiufupi wasifu wake ni mchaga wa Uru.
Dhamira yangu ni kuanza nae maisha kama mke na mume endapo Mungu ataendelea kutuonesha upendo huu.
Kama mjuavyo kwa hili kabila maranyingi hukosi pingamizi za hapa na pale.. Ila kwangu sio issue sana.
Sasa katika harakati zangu za kiume kama mwez mmoja hivi ulopita nikakutana na msichana mwingne... Nikaanzisha mawasiliano nae so, kukawa na chatting za hapa na pale bahati mbaya mtt wa watu kanogewa kanifungukia...
Labda niseme kitu kutoka ndani ya nafsi yangu jins nilivyo, ni mpole sana na sipendi kupindisha ahadi niloiweka kwa mtu. Nakua na huruma sana na mtu, tofaut na ninavyojijali mwenyewe.
Sasa nae huyu binti ananiletea swaga za kuishi pamoja na kuanza maisha. Na amefika mbali zaid kunitambulisha had kwa wazaz wake, kitu ambacho sikutegemea na had wazaz wakaniita nikawasalimu, na Mimi kwa heshima ya wazazi nikaitikia wito, tukasalimiana.

Kitu ambacho kinanitesa hapa ni jinsi ya kujitoa kwa huyu binti wa pili, bila kuumiza nafsi yake kwan kila nikifikiria mipango nilopanga na huyu mchga wangu na sipend kuitelekeza, napata kigugumizi. Sipend kumuumiza kihisia sabab sipend kuona mtu anateseka kwa ajil yangu.
Na huyu mchga nikitania tu kusema ile tuachane ni pressure na kuumwa siku nzima.
Labda mnipe ushauri wanajamvi ni njia gan sahihi, ya kujikwamua hapa. Kinachonipa Mawazo zaid ni kwamba huyu mchaga nilimtafutia kazi mahali, na mwezi ujao ndo anakuja, so najua kutakua na mizengwe ya hapa na pale sabab ni mfuatiliaji sana na huwa sipend kujificha kweny chatting zangu so atagundua tu. Najua kwa umri wetu huu 25s...ni wachache wanaofikia zaidi ya miaka mitatu, wakiwa pamoja.
Nisaidieni nitoke kweny mawazo haya... Au wapi nilikosea au kipi nikifanye ambacho sitamuumiza mtu.
Best Regards
 
Usihofie wachaga, wahaya baba, Upendo hauchagui kabila.

Hapa naona umekosa kuwa na msimamo thabiti kama mwanaume na nini unataka kwa wakati gani. Rekebisha hilo kwanza.
 
Usihofie wachaga, wahaya baba, Upendo hauchagui kabila.

Hapa naona umekosa kuwa na msimamo thabiti kama mwanaume na nini unataka kwa wakati gani. Rekebisha hilo kwanza.
Sio kwamba nimekosa msimamo, shida ni speed ya huyu wa pili, ambayo imenifanya nibak mdomo wazi na kusindwa kujitoa kwake
 
Sio kwamba nimekosa msimamo, shida ni speed ya huyu wa pili, ambayo imenifanya nibak mdomo wazi na kusindwa kujitoa kwake
Ndio kukosa msimamo kwenyewe unamtaka wa kwanza na una malengo nae thabiti, kwanini umejipeleka kizembe kwa wa pili? ulikuwa na uwezo wa kukataa ulipoitwa na wazazi wake sasa ulikwenda jichimbia zaidi kaburi lako mwenyewe.
 
Sio kwamba nimekosa msimamo, shida ni speed ya huyu wa pili, ambayo imenifanya nibak mdomo wazi na kusindwa kujitoa kwake
ukaona umeongea point hapo huyo jamaa aliyekuambia huna msimamo hajakosea, ushajijua hutaki mtu ateseke kwa ajili yako ikawaje sasa uanzishe mahusiano mapya??

sina ushauri mimi haya mambo yamezidi umri wangu
 
Labda niseme kitu kutoka ndani ya nafsi yangu jins nilivyo, ni mpole sana na sipendi kupindisha ahadi niloiweka kwa mtu. Nakua na huruma sana na mtu, tofaut na ninavyojijali mwenyewe.
[emoji121][emoji121][emoji121][emoji121][emoji121]

Mkuu punguza ubaba huruma wako na usiendelee kutongoza hovyo huruma yako itakuponza baki na mchaga wako
 
Eti ubaba huruma hehe!
 
Mkuu kuoa mchaga ni kujilipua but upendo hauna mipaka.Kimsingi wewe umekosa msimamo ilitakiwa huyo wa pili umwambie kuwa space zimejaa.
Sasa andaa siku tu na uwe na balls za chuma kama mwanaume mchane huyo mpenzi wako wa pili kuwa una mtu.
If you don't hurt early, you will hurt later and badly.
Goodluck mkuu na manka wako.
 
Acha uzuzu ulifahamu fika kua unamtu alafu ukaamua kukubali Huyo wa pili aingie kwenye maisha yako, alafu unasema unahuruma NOP wewe huna huruma ila ni katili namba moja kwa ulichofanya unafikiri Huyo mchaga wako akijua atajisikiaje?
Huyo wa pili mwambie ukweli kabla jipu halijatumbuka na likatengeneza donda kubwa
 
Cjui kwann huwa cwaamini wanaume walio chini ya 30 wanakuga bado hajakomaa kifikra kama mtoa Mada apo juu.....
Yan unamuwekea mazingira demu adi anakufungukia adi home anakupeleka mhh kama hukua na nia nae usinge endelea kumuintertain...
 
Mkuu kuoa mchaga ni kujilipua but upendo hauna mipaka.Kimsingi wewe umekosa msimamo ilitakiwa huyo wa pili umwambie kuwa space zimejaa.
Sasa andaa siku tu na uwe na balls za chuma kama mwanaume mchane huyo mpenzi wako wa pili kuwa una mtu.
If you don't hurt early, you will hurt later and badly.
Goodluck mkuu na manka wako.
Fantastic reply
Thnx much
 
Back
Top Bottom