Mkopo anapata kama kawaida kama alishapewa na ikiwa anabadilisha kozi ndani ya chuo hicho hicho!! Ila utambue bodi hupata taarifa ya kozi unayosoma (muda) na hivyo hupanga kiasi cha mkopo mpaka pale unapomaliza! Sasa basi, we kama kozi yako ya awali ilikuwa miaka 3 basi fanya exchange na kozi ya miaka 3 ili kama unategemea mkopo usije teseka baadaye, kwa maana kama ulichaguliwa kozi y miaka 3 na ukapata mkopo kisha wewe ukaamua kubadilisha kozi na kuchagua kozi ya miaka 4 basi huo mwaka wa nne utakuhusu kwa kila kitu!! Hayo niliyaona nilipokuwa St Augustine University of Tanzania -Mwanza Campus, sijui kwingineko, ila pia naamini kwamba Bodi ya Mikopo wanaruhusu!!
:bowl:Nimewasilisha!!!:A S-cry: