Msaada wa kufukua mwili wa marehemu

chakka

Member
Oct 28, 2012
21
13
Tafadhali naomba kifungu cha sheria kinachoruhusu kuomba kibali cha mahakama kwa ajili ya kufukua mwil wa marehemu kwa uchunguzi zaidi.
Nawasilisha tafadhali.
 
Tafadhali naomba kifungu cha sheria kinachoruhusu kuomba kibali cha mahakama kwa ajili ya kufukua mwil wa marehemu kwa uchunguzi zaidi.
Nawasilisha tafadhali.
Anayechunguza ni wewe mwenyewe?
 
Labda jitambulishe ujulikane vizuri. We ni nani? Kazi yako nini? una taaluma gani? Na je uchunguzi unaoutaka kuufanya unahusu jinai au ni personal interest?
Sio vema sana kuweka wazi kila kitu ila nipo kwenye taasisi ya serikaili napeleleza suala hill awali marehemu alionekana kama amejiua ndugu wakamzika ila baadae walipata taarifa kuwa ameuwawa hivyo kutaka uchunguzi wa kina ufanyike
 
Kama kesi mojahuko mbeya imehukumiwa juzi na mahakama kuu.

sasa kama upo kwa gov agency, si mkuu wako wa kazi yupo? Unataka kusema amekuachia kila kitu? Kwa ninanvyofahamu, lazima atokee mtu wa kutoa hayo malalamiko naaende kutoa maelezo polisi, atahojiwa kwa kina kwa nini anahisi marehemu hakujinyonga bali aliuliwa kisha kutundikwa mtini na kitanzi kama ilivyotokea huko mbeya, ataeleza anayemtilia shaka kufanya unyama huo, polisi wakiridhika na maelezo yake, ndio watafuata taratibu zakisheria mwili ufukuliwe, na madaktari ndio watafanya uchunguzi huo mbele ya askari polisi na wanandugu, taarifa ya daktari ndiyo itaamua kesi kufunguliwa na wahusika kukamatwa kuendelea na kesi hiyo.

Mtu binafsi huwezi kuruhusiwa kumsumbua marehemu, labda kikao cha wanandugu kuomba kwa hakimu kibali cha kufukua kwa lengo la kwenda kuzika sehemu nyingine, siyo kufanya uchunguzi
 
Inawezekana, Mimi nilihamisha mwili wa baba angu takribani baadaya ya miaka 30 kuzikwa, unatakiwa uende polisi wilayani aliko zikiwa, uwe na barua ya balozi inayoeleza kwa nini unataka kufanya hivyo.
 
Hiyo kazi mwachieni Yesu atamfufua sikuya mwisho katika ufufuo wa wafu woote! Kwa sasa mwacheni marehemu apumzike kwa amani ya Bwana...
 
Back
Top Bottom