Msaada wa kuchukua fedha zangu NSSF

Msaada wa kuchukua fedha zangu NSSF

kachabali

New Member
Joined
Apr 26, 2016
Posts
4
Reaction score
0
Nafanya kazi shirika fulani, lakini tatizo limekuja sehemu moja mimi na hawa NSSF,

Mkataba wangu umeisha tarehe 30/2/2016, bahati mbaya niliondoka kwenda kwenda nyumban bado barua za kusimamisha kazi na barua za kuchukulia mafao yangu zilikua hazijakamilika, na kwa kuwa nilikua na haraka ikabidi niziache kwa dhumuni kuwa nitarudi nitazikuta, mkataba uliisha lakini nilisaini mwingine kabla sijaondoka, nipo nyumban bado mshahara ulikua unaingia kama kawaida,

Tatizo limekuja jana nimeenda kutoa wananiambia kuwa siwezi kutoa pesa hiyo kwa kuwa bado mafao yanaingia kama kawaida, na baada ya kuchangia bado kuna pesa tayari imeingia ambayo ni ya mwezi wa 3 na 4, hivyo inaonesha bado nipo kwenye system kama kawaida, nikawaambia lakini mkumbuke ninayo barua yangu ya mwezi huo kukoma, na pia hiyo pesa mnayosema imeingia mimi sina mpango nayo bali naitaji pale nilipoishia basi, wamegoma.

Naombeni msaada kuhusu hili, siruhusiwi kuchukua pesa wakati mafao yameingia mengine?
Pili nina barua ya office pia na viambatanisho vyote, naomba msaada kuhusu hili
 
Kwa staili yako hiyo nadhani mfuko ungekuwa umeshakufa/kufilisika kabisa!.
Nadhani ni wakati sasa NSSF kupitia SSRA wakatoa mwongozo wa hili fao la kujitoa!
Watu wamekuwa wakiacha Kazi ili kujipatia Pesa na baada ya wiki mbili wako Kazini!
Ule mfumo wa Zamani wa kusubiri miezi tatu sijui sita umeishiaga wapi?
 
Kwa hiyo wewe umeacha kazi lakini bado mshahara unaingia?, wewe ni jipu subiri kutumbuliwa kwa staili ya wafanyakazi hewa
 
Kwa hiyo wewe umeacha kazi lakini bado mshahara unaingia?, wewe ni jipu subiri kutumbuliwa kwa staili ya wafanyakazi hewa
sijaacha kazi mkuu ila nikua kazi ninayofanya ni seasonal,ivyo kla mwaka narenew mkataba mpya,
 
Kwa staili yako hiyo nadhani mfuko ungekuwa umeshakufa/kufilisika kabisa!.
Nadhani ni wakati sasa NSSF kupitia SSRA wakatoa mwongozo wa hili fao la kujitoa!
Watu wamekuwa wakiacha Kazi ili kujipatia Pesa na baada ya wiki mbili wako Kazini!
Ule mfumo wa Zamani wa kusubiri miezi tatu sijui sita umeishiaga wapi?
boss nafanya kazi kwa msimu,ivyo ukisha narenew
 
Ungehama mfuko baada ya kuacha kazi
Hili ndo wazo la kulifanyia kazi msimu ujao,

Kuna 40M zangu nadai LAPF wamenzingua kwa ajili hii hii, next time naacha kazi nahama mfuko nikusanye mafao yangu yooote
 
Mkuu pole, hapo huwezi pata hiyo pesa, sheria iko wazi mafao ni kwa mtumishi aliyeacha/kuachishwa kazi, ulitakiwa unaposign new contract umwambie mwajiri wako aweke pending mafao yako yote ya mkataba mpya hadi pale utakapomwambia aanze kukuwekea. Ikionekana unachangia hata kama ni mifuko mingine huwezi kupewa hiyo pesa. Usipoteze muda subiri ukiacha hiyo kazi utafungua mafao yako yote, usidanganyike kumpa mtu rushwa ili akufanyie mpango, atakulia pesa yako na mafao hutopata.
 
Hili ndo wazo la kulifanyia kazi msimu ujao,

Kuna 40M zangu nadai LAPF wamenzingua kwa ajili hii hii, next time naacha kazi nahama mfuko nikusanye mafao yangu yooote
Ukihama mfuko haisaidii, sa hivi mifuko yote ya jamii wanatumia system moja, na wanatress kama unachangia mifuko mingine, njia nzuri ni kuweka pending malipo yako pale unpopata ajira mpya hadi pale utakapolipwa ndo unamwambia mwajiri wako aanza kuchangia.
 
sijaacha kazi mkuu ila nikua kazi ninayofanya ni seasonal,ivyo kla mwaka narenew mkataba mpya,
Kwa nini unataka kuchukua sasa, si wanasema hizo ni huko mbele na zinakusaidia kupata zile pesa za uzeeni baada ya kustaafu kazi (nimezisahau sijui wanaziitaje vile).
 
Back
Top Bottom