Asante mkuu kwa ushauri wako.Hilo linawezekana sana tu sema ishu inakuwa ngumu kubadilisha mpaka vyeti vyote. Duuuh!
Aende mahakamani apewe utaratibu wa kubadilisha majina. Atoe na sababu nzito nzito za kutaka kubadilisha jina.
BTW, sioni mantiki ya yeye kubadilisha majina na ukubwa wote huo. Better ajaribu kuapply cheti kingine cha kuzaliwa kuliko kuchukua process ndefu mpaka kuifanikisha.
Mwacheni atumie majina ya mjomba kma fadhila kwake kwa kumsaidia katika mambo yote hayo.
Wasiwasi wake upo kwenye visa hapo mkuu, mambo ya cheti na baba au mama na hayo mambo mengine haiwezi kumsumbua kweli? Na ndio kitu hata mimi ilikua namuawazia!!why all the trouble?? Kwa uzoefu wangu mdogo....Ni ngumu kiasi kubadili majina yakaweza kuonekana kwenye nyaraka zako zote muhimu. Kwa mfano kwa vyeti vya taaluma ukishafanya mtihani wa form four jina linakuwa kama fixed fulani hivi. Birth certificate unaweza uka-manouvre ukapata pale RITA ambapo utaweza pia kupata passport na visa etc, pia kwa mwajiri siku yoyote ukihitaji kujulikana vyovyote unaenda kwa wakili unaleta kiapo wanakubadilishia - hii wanafanya sana hata wanawake wanaoolewa. Ngoma ipo kwenye vyeti vya kitaaluma, na kwa hiyo utaishi maisha ya kujieleza kila mara ili watu wasikutuhumu kuwa umefoji!
This is the answerAwaone Wanasheria watamsaidia kumuandalia Deed Poll for change of name(s) Kisha ataipeleka kwa Kamishna/ Msajili wa kumbukumbu na nyaraka kwa ajili ya kupata usajili
Yes asante sana sana , angalau tumejua nini na wapi pa kuanziaMkuu,
Kisheria, kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, haja yako inatatuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Viapo (the Oaths (Judicial Proceedings) and Statutory Declarations Act.) Unachotakiwa kufanya ni kuandika nyaraka ya kisheria ambayo inajulikana kama "Deed Poll" ambayo ni nyaraka mahususi yenye kukuwezesha kutimiza hiyo haja yako ya kubadilisha majina. Nyaraka hiyo inapaswa kugongwa muhuri na Kamishna wa Viapo (Wakili, Hakimu, n.k.) kisha unaipeleka kuisajili kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Hati/Nyaraka (The Registration of Document Act ) ambapo kwa hapa Dar es Salaam ni pale Wizara ya Ardhi.
Nafikiri angalau nimekupa mwangaza.
Kaka ...