Nenda ofisi za mkoani idara ya elimu mkoa aliopangiwa ukifika uandike barua wewe kama mzazi unataka umuhamishe mtoto wako kwenda tabora uweke na sababu ya kufanya hivyo,
Barua yako Wala haiendi popote na wala haina maana sema tu itatumika kutoa maelezo ya wao kukuandikia barua ya uhamisho.
Watakuandikia barua ya uhamisho utaenda nayo Tabora mokani ukifika watampangia shule unayotaka(watakuanfikia barua ya kumpangia Tabora Girls) mtoto ataripoti ila uhamisho utakuwa Bado haujakamilika,
Uhamisho utakamilika badae baada ya wanafunzi kuripoti wote ndo prems namba zao zitatoka iyo namba utafanya mawasiliano na mkuu wa shule alikopangiwa awali(prems namba yake itatokea huko) airuhusu iondoke halafu aitume shule anayohania wai add hapo ndo uhamisho utakuwa umekamilika.