Msaada wa kiufundi katika gari hili

Mbassa jr

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,234
3,172
Gari ni Verossa..

Ni automatic transimission, tatizo lake ni kwamba naweza nikatembelea vizuri tuu ila ikifika sehemu ya kupunguza spidi labda kwenye tuta au korongo, nikishataka kukanyaga tena mafuta unakuta RPM inafika mpka 3 na gari inakuwa haisogei bali inakuwa inaunguruma tuu afu ghafla inashtuka na RPM inashuka mpaka normal ndo inaanza ku-gain spidi upya.

Je, tatizo laweza kuwa ni nin?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una mtindo wa kushift kutoka D kwenda N? wakat wa ku drive?

Je.. gearbox service ulifanya mara ya mwisho lin..?

Ushauri..

Tatz moja kwa moja ni Gearbox so tafuta mtaalam wa gearbox aichunguze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Engine kuna gia ina ng'anng'ania au kwenye gia box mfumo wa cluch hakiachii vizuri tafuta fundi akague gari lako kabla matatizo hayajawa makubwa
 
Tatizo ni kwenye gearbox ila kabla ya kuingia ndani,iangaliwe transmission control module, kifaa cha electronic mara nyingi ni nje ya gearbox ambacho ndicho kinatoa maelekezo toka kwenye pedal kushirikiana na on board computer kujua ni gear ipi itumike kutokana na nguvu uliyokanyaga.
 
Nina wasiwasi una tatizo la control module ktk gearbox yako,jaribu kutafuta hicho kwanza kabla hujagusa gearbox yenyewe
 
Hapana sina mtindo huo kbisa isipokuwa sijachange gearbox oil muda mrefu kdgo sasa sijajua inaweza kuwa ni tatzo Gentlemen_,

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo linaanzia hapa kiufupi au kwa msaada wa ushauri unatakiwa kubadilisha atf yako angalau kila baada ya km 20,000 kama gari inatembea in severe conditions na kubadili kila baada ya km 60,000 kama gari inatembea in normal condition na hizo km uchange kama tu umeweka atf specific kwa ajili ya gari hiyo sio uende huko kwa mafundi wakuwekee international atf mbovu hazina viwango vyovyote uisukume ndiga hadi izingue halafu uje huku uanze kusema nilisema ubadilishe kila baada ya mda fulani hiyo no na verosa hiyo atf ni 100,000- 90,000 kulingana na ulipo so jipange
 
Back
Top Bottom