Msaada wa Kisheria

Msaada wa Kisheria

Magehema

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
428
Reaction score
28
Nilipata bahati ya kuona mkataba wa mchezaji mmoja wa moja ya hizi timu zetu pendwa mwaka huu wa usajili. Mchezaji huyo alitakiwa kuusaini huo mkataba uliokuwa ukionyesha kwamba atalipwa kiasi cha kama milioni 15 kama pesa za usajili na pia atakuwa napokea mshahara wa kiasi cha mil 1.5 kwa mwezi katika kipindi cha miaka miwili ya mkataba wake.

Kilichonishangaza katika mkataba huo ni kipengele ambacho kinasema iwapo mchezaji huyo atataka kuuvunja huo mkataba atahitajika kulipa kiasi cha dola za marekani 600,000.

Swali: Iweje mkataba ambao thamani yake haizidi hata Shilingi Milioni 60 za kitanzania [usajili 15 million + mshahara 1.5mil X 24 = 51,000,000] uvunjwe kwa mabilioni ya shilingi???

Msaada wanasheria
 
Back
Top Bottom