Msaada wa kisheria

Msaada wa kisheria

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Ndg zangu nawasalimu wote amani iwe kwenu!

Naomba kupewa ushauri wa kisheria kwa jambo kama hili, mfano kama baba na mama wamepata mtoto na ili kuzuia kupata mtoto mwingine ndani ya muda mfupi wakaamua kwenda hospitalini/ dispensary au kituo cha afya kutaka ushauri na kisha kupewa ushauri na mtaalamu kama nesi au doctor kutumia njia za kisasa kupanga uzazi. Wahusika yaani baba na mama wakakubali na mke kuwekewa KITANZI lakini katika uwekaji yule mhusika akakosea kukiweka yaani akaweka vibaya huku mteja akiamini amewekewa njia madhubuti ya kuzuia kupata mimba nyingine ya haraka, kisha ndani ya muda mfupi mhusika anagundua ana mimba nyingine baada ya dalili za hapa na pale na klsha kuthibitisha kwa kupima na kugundua kwamba kweli mimba ipo. Mteja aliporudi kujua imekuwaje kapata ujauzito wakati aliwekewa kitanzi na bado kipo ndani na tena kiliwekwa na mtu aliayeaminiwa kwenye kazi hiyo, dokta katika kuchunguza akagundua kwamba nurse alikosea kukiweka hali liyoplekea mhusika kupata ujauzito nje ya muda aliotaka yeye.

Katika mazingira kama haya mhusika anakuwa ameathirika kwa mengi kwanza kuwa na ujauzito katika muda ambao hakupanga, kuwa na ujauzito mtoto wa awali angali bado ni mdogo sana, kuharibu ratiba za kikazi na kimalezi za wahusika, kuathirika kisaikolojia na kiuchumi na wakati mwingine kuonekana mtu wa ajabu mbele za jamii. Sasa je katika mazingira haya nini haki ya muathirika ? je ana uwezo wa kufungua mashtaka dhidi ya mtaalamu au hospitali husika? . Najua mambo kama haya ya kufungua kesi kwa mazingira kama haya ni mageni katika nchi yetu lakini je kisheria muathirika ana haki?

Ushauri wenu ni muhimu ili kuongeza uelewa na kutatua changamoto hii.

Nawasilisha

Bringbackbrothermoalive.
 
Nahisi unaweza lakini naamini MPANGO WA MUNGU TU mkuu muache mtoto akue huwezi jua kusudi la Mungu.SAMEHE TU.
 
Ngoja tutakujibu mkuu, kwasasa Tupo busy na Hotpot za Lunch tulizotoka nazo home
 
Kabla hujawekewa njia ya uzazi uliochagua unapewa elimu ambapo utaelezwa pia kuna uwezekano wa asilimia fulani kupata mimba
 
Nahisi unaweza lakini naamini MPANGO WA MUNGU TU mkuu muache mtoto akue huwezi jua kusudi la Mungu.SAMEHE TU.

Mkuu aksante kwa ushauri mzuri hata hivyo kuna wakati uzembe unasababisha madhara kwa watu au jamii kisha tunasema ni mpango wa Mungu. Kwangu mimi kulea mimba na mtoto siyo hoja maana wazazi wangu walitulea 8 kwa maisha ya chini kuliko niliyonayo sasa ila uzembe huu unaweza kukomeshwa tunapochukua hatua
 
Ngoja tutakujibu mkuu, kwasasa Tupo busy na Hotpot za Lunch tulizotoka nazo home

Mkuu unaenda job na Hotpot ya lunch!!!! mkuu mimi mihogo za mama ntilie zimenitosha hapa kiungulia kama yote ,hongera sana bosi
 
Kabla hujawekewa njia ya uzazi uliochagua unapewa elimu ambapo utaelezwa pia kuna uwezekano wa asilimia fulani kupata mimba


Mkuu ni kweli ila kwahili doctor kasema nurse alikosea na alimwita huyo nurse na kumuonesha makosa yale pale mhusika alipoenda kujua sababu ya mimba wakati kitanzi kingali ndani.
 
Sue the Hospital joining the nurse for professional negligence as a tortious liability, then weka damages za kutosha.
 
Sue the Hospital joining the nurse for professional negligence as a tortious liability, then weka damages za kutosha.

Ndiyo nilitaka kujua katika sheria zetu hapa nchini kunako Jamhuri hii sheria zinaruhusu kesi kama hizo?, je kuna kesi yoyote kama hii iliyowahi kutolewa maamuzi?
 
In medical science all things or nearly all things are uncertain. THAKE VS MAURICE [1986] 1 ALL ER 497.

But i think you can succeed on suing the practitioner for neglegence for having failed to warn you on possibility of getting preg.
 
Ndiyo nilitaka kujua katika sheria zetu hapa nchini kunako Jamhuri hii sheria zinaruhusu kesi kama hizo?, je kuna kesi yoyote kama hii iliyowahi kutolewa maamuzi?
Theodoclina Alphaxad v. Medical Officer in Charhe of Nkinga Hospital [1992] TLR 235
Whiteside v. Jasman [1971] HCD n. 88
Paul S. Albert Itule v. Theresia Andrea [1980] TLR 98

Those are cases in Tanzania relating to a tort of negligence.

Just find a lawyer and everything will be fine.
 
In medical science all things or nearly all things are uncertain. THAKE VS MAURICE [1986] 1 ALL ER 497.

But i think you can succeed on suing the practitioner for neglegence for having failed to warn you on possibility of getting preg.

Thank you brother let me talk to law practitioners and my relatives to see what I can do to discipline mtu.
 
Theodoclina Alphaxad v. Medical Officer in Charhe of Nkinga Hospital [1992] TLR 235
Whiteside v. Jasman [1971] HCD n. 88
Paul S. Albert Itule v. Theresia Andrea [1980] TLR 98

Those are cases in Tanzania relating to a tort of negligence.

Just find a lawyer and everything will be fine.

Thank you man
 
Thank you man
The doctor owes a duty of care to his patients as was seen in the case of Theodoclina Alphaxad
v Medical Officer in Charge of Nkinga Hospital

. In this case Nkinga hospital was held liable
for causing amputation of the minor’s hand due to the negligence of the doctor on duty. The court
of Appeal of Tanzania on this case established the following factors that the doctors instructions
to the patient’s father was sufficiently to prove there was a relationships and the doctor owes a
duty of care to the minor and the father was not properly informed of the serious risk to his
daughter.
 
Back
Top Bottom