Msaada wa kisheria

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,305
12,600
Amani na iwe kwenu wanasheria wa jf

Naomba ushauri wenu wa kisheria kuhusu hili:

Niliwahi kumpa ujauzito binti mmoja mwaka 1982, watu wengi kwenye kijiji kile pamoja na wazazi wake walikuwa wanaufahamu uhusiano wetu. Kwakuwa mimi nilikuwa masomoni yule mama akaona bora ampe ule ujauzito kijana mwingine ambae alikuwa akimtongoza wakati alipokuwa na mimi kwenye uhusiano. Baada ya kuona mimi niko masomoni akaona heri atembee na yule kijana angalau mara mbili tatu ili apate uhalali wa kumpa ile mimba.

Baada ya miezi miwili ya kuwa nae kwenye uhusiano yule msichana akagundulika kuwa ni mjamzito. Wazazi wake walipomtaka ataje nani amempa ujiuzito ule yule msichana akamtaja yule kijana badala ya kunitaja mimi ninaefahamika na wengi kuwa nina uhusiano nae wa kimapenzi.

Yule kijana baada ya kusikia msichana ana mimba na amemtaja yeye akakataa na akatoroka pale kijijini. Hata hivyo kutokana na ukali wa wazazi wa msichana walilazimisha kumfungisha ndoa na mdogo wake yule kijana aliyetoroka. Yaani amemuolea kaka yake, baada ya hali kuwa hivyo baba mzazi wa wale vijana ilibidi akamtafute mtoto wake huko alikotorokea ili aje atunze mkewe ambaye ameletwa nyumbani kwao. Kijana kusikia hivyo alikubali kurudi nyumbani na kumkuta mkewe.

Mama alijifungua mtoto wa kike ambaye alirandana sana na mimi na dada zangu, hivyo kumfanya yule kijana ahisi kuwa yule mtoto ni wangu sio wake kwakuwa hata yeye alikuwa akiufahamu saana uhusiano wangu wa kimapenzi na yule msichana kabla yeye hajatembea naye. Watu nao pale kijijini walikuwa wakimtania kuhusu yule mtoto kuwa sio wake.

Mtoto alipofikia umri wa miaka 4 majirani na wajomba zake walianza kumwambia kuwa hule baba sio baba yake. Hii ilisababisha yule baba yake asimpeleke shule kwa sababu hiyo, eti hawezi kumsomesha mtoto ambaye siyo wa kwake. Mtoto yule hakusoma kabisa na alimuoza mume akiwa mdogo kabisa. Mizozo ya kifamila kuhusu yule mtoto hata mama mzazi ilibidi amueleze mtoto wake ukweli kuhusu baba yake halisi. Yule mtoto nae amemueleza mume wake na watoto wake kuhusu habari za mzazi wake halisi na wote wanafahamu.

Sasa yule mama ni mtu mzima na ana watoto 6, sasa hivi anasema anamkana yule baba yake anasema anataka kuja kwangu kama baba yake halisi. Alianza mkakati wa kutaka kurudi kwangu kwa kuja kwa wazazi wangu na dada zangu na kutafuta namba za simu za watoto wengu na kuwaeleza kuwa yeye ni ndugu yao. Hata hivyo wazazi na ndugu zangu wengi walikuwa wanalifahamu suala hivyo hivyo hawakushtuka sana.

Yule baba aliposikia kuwa yule "mtoto wake" anataka kurudi kwa baba yake mzazi anamtishia kuwa huwezi la sivyo nitakuua. Lakini mtoto amekazana anasema anataka kuruja kwangu kwakuwa yeye sasa ni mtu mzima haogopi kurekebisha makosa tuliyotenda huko nyuma juu yake.

Ninaomba ushauri kujua kama

1. Je, yule mtoto afanye nini ili aweze kutimiza azima yake ya kutaka kuja kwangu?
2. Kuna madai yoyote yanayoambatana na uwamuzi huo wa mtoto?
3. Yeye (mtoto) ni mtu mzima sasa ana mumewe na watoto 6, je, kuna umuhimu wa kuomba ruhusa kwa yeyote kuja kwangu?
4. Kuna kosa lolote kwangu, mama yake au yule mwanaume wa mtoto kwenye tukio hili?
5. Mtoto atatenda kosa gani kama ataamua kuja kwangu sasa hivi?
6. Mimi nitatenda kosa gani kama nitampokea au kumkataa mtoto?
7. Nini kifanyike ili haki itendeke na ionekane ikitendeka?

Nawasilisha.
 
Mkuu pole sanaa, najua ulikimbia kwa purpose kule kijijini na haukua na lengo la kumkana mtoto, kwa bahati mbaya sanaa sheria zetu zinamtambua mtoto kua ni binadamu yoyote mwenye umri wa miaka 18 kama likitokea la kutokea kwa wakati huu, uyo baba mwingine anajitaftia matatizo tu ya kijinga hasa anavyotishia kuua, ifahamike huyu sasa sio mtoto ni mtu mzima ambae ana haki ya kuchagua jamii flani ajiunge nayo au lah, hakuna sheria yoyote hapa nchini inayoweka mipaka ya machaguzi ya kimahusiano, kindugu au kijamaa akija kwako ni haki kwake na hapaswi kuomba au kujaza fomu yoyote mahakamani isipokua tu kama ata taka kubadilisha majina yake yawe yanaishiwa na jina lako na la ukoo wake, mzazi hana umiliki wa mtoto wake tena endapo uyo mtoto akiwa ni mtu mzima na ndio maana sheria ikagusia ukomo wa uangalizi wa mzazi kwa mtoto, sasa mtu mwenye watoto 6 na umri karibu miaka 35 hapaswi kufanya lolote kati ya uliyoagizwa.

Kama kungekua na mambo ya kimila unapaswa kufanya kumuhalalisha uyo awe mtoto wako basi ungefanya hivyo kwakua sheria mwisho wa siku itataka connection ya ubaba wako kwa huyu mtu ambae ni mtoto wako hasa yanapotokea majanga mengine kama mgogoro wa ndoa ya uyo mtoto au mambo ya misiba hayo.
 
Asante sana mkuu kwa maelezo haya, nilikuwa naogopa kumkaribisha nyumbani
 
Back
Top Bottom