Mr Suprize
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 864
- 947
Wakuu poleni na majukumu ya kulijenga taifa.!
Nina dada yangu amekumbwa na tatizo ambalo linaweza kumpelekea akafungwa kama msaada wa kisheria hautapatikana haraka.
Nianze kwa kueleza historia fupi ya huyo dada angu.
Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari alienda mjini kufanya kazi ya kuuza duka la vocha za jumla na rejareja duka ni la afisa elimu wa mkoa. kadri siku zilivyokuwa zikiendelea huku akiwa anafanya kazi ya duka alibahatika kutoka kimapenzi na mwanaume mmoja ambapo kadri siku zilivyozidi kwenda walibahitika kupata mtoto wa kike.
malezi ya mtoto yaliendelea vizuri na huyo mwanaume alikuwa anatoa huduma kwa mtoto kama kawaida.
Baada ya muda kidogo iligundulika yule mwanaume ameoa huku akimficha dada yangu asijue kama anaishi na mke. baada ya dada yangu kugundua kuwa baba wa mtoto wake ni mume wa mwanamke mwingine aliamua kumuacha yule mwanaume, kitendo ambacho mwanaume hakukubali aliendelea kung'ang'aniza waendelee kuwa wapenzi hata kama yeye ana mke.
Dada yangu aliendelea kukataa huku mwanaume akilazimisha kwa kumpiga na kumjeruhi vibaya mpaka kupelekea dada yangu kulazwa hospitali mara nyingi kwa kipigo.
Mambo yaliendelea hivyo mpaka mwaka jana desemba mwishoni dada yangu aliamua kuacha ile kazi ya kuuza vocha na kurudi kijijini kuendelea na maisha mengine ya amani na furaha. Mtoto waliyezaa anaitwa Angel ana umri wa mwaka mmoja sasa. MWISHO WA HISTORIA FUPI.
Niendelee, hapo chini nimecopy na kupaste meseji ambazo nilitumiwa na huyo dada angu leo tarehe 02/February zikieleza tatizo alilonalo baada ya kuacha kazi.
" Ni hv baada ya kuacha ile kaz ..alikuja ba enjo had nnapokaa akaniambia kua yy hawez kuachana na mm, akanyang'anya cm akatoa lain yangu na kuondoka nayo, pia alikua anakuja nyumban na kunilazmisha kufanya nae mapenz nikikataa ananipga...bas mm nlivoona kaz cna nikaamua kukusanya vitu vyangu ili nirud kijijin... baada ya kurud yy alivockia akaja had kijijini na kunitafuta had akanipata ila hatukuongea maana me nlvomuona nlikataa kwenda alipo yeye kumbe alikua anamalengo yake,
akaenda kushtak kituoni kua mm nilikua mke wake na nimetoroka na nimemuibia vitu vyake vingi..ndo wakaja askar kunikamata kwenda kituo cha polisi, tulvofka pale ye akaondoka me nkabak,nikaulza tatzo nn wakaxema unakesi ya wizi na imefunguliwa mjini kwahyo inabd ukae lockap had watakapofika askar wa mjini kunichukua, nikakaa pale cku 3 kwan dhamana walinikatalia had jana alivofika mkuu wa kituo na kusikilza maelezo yangu ndo akatoa dhamana na mm nikarud nyumban, ndo leo axubuh nkaenda kuripot na tukatoka na askar na kuja huku mjini ambapo nimewekewa mdhamana na kesho tunaenda mahakamani..maana nimekana kosa, kaandika vyombo vyote vya ndan nilivyonavyo had vijiko,vyeti vyake vya darasa la 7, kad ya benk, na kad za biashara..tv, sabufa, pas ya umeme had viatu vya mtoto, nmekataa kwamba ckua naish na huyo mtu pia vitu ni vyangu nimenunua mwnyw na walioniuzia wapo..""
MWISHO WA UJUMBE WAKE UNAOELEZA TATIZO alilonalo.
Naamini wengi wenu mmenielewa labda kwa kuongezea tu dada angu alikuwa amepanga chumba na alikuwa anaishi na mwanae tu na pango alikuwa analipa mwenyewe kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya. huyo mwanaume hajawahi hata kupeleka barua nyumbani kuhusu kumwoa dada angu.
Ninachoomba ni ushauri wenu uwe wa kisheria hata wowote ule ilimradi dada yangu awe huru maana kesi anayotuhumia ni ya wizi wa vifaa na hivyo vitu dada angu ni vyake japo alinunua kwa watu na hana risiti.
Nitangulize shukrani zangu za dhati!