Msaada wa kisheria unahitajika hapa

Anko Elly

Member
Feb 22, 2017
69
70
Hivi Kama una ndugu, jamaa au rafiki ambaye anafanya biashara ya kuuza bidhaa.

Lakini ghafla anakuita anakwambia kwamba ana biashara Kubwa ambayo itahitaji kupitia kwenye akaunti ya benki.

Kwa kuwa mnafahamiana, ukaona isiwe tabu, hapo biashara umedokezewa kdg na percentage ushaambiwa utakula ngapi.

Lakini katika hali ya sintofahamu unakuja kutaharuki ile biashara imeingia dosari, wakati huo pesa imeshatoka na hela ameshachukua na changu nimeshapewa.

Kumbuka wakati wa hiyo biashara inafanyika alikuwepo mwanasheria pamoja na sisi wahusika, ambao wote kwa pmj tuliamwaga sahini zetu.

Linapokuja suala la kesi hapo nani mwenye makosa? Je, mwenye akaunti anauwezo wa kuingizwa hatiani?

Msaada wenu tafadhali
 
Hiyo ni kesi ya money laundering.

Kwa nini mtu mwenye biashara kubwa asitumie akaunti yake atumie akaunti ya mtu mwingine?

Mwenye akaunti anaweza kuwekwa hatiani kwa money laundering hapo.

Na huyo mwanasheria anaweza kuchukuliwa hatua kuwezesha money laundering kinyume cha sheria kama ikionekana sheria zimevunjwa.
 
Hiyo ni kesi ya money laundering.

Kwa nini mtu mwenye biashara kubwa asitumie akaunti yake atumie akaunti ya mtu mwingine?

Mwenye akaunti anaweza kuwekwa hatiani kwa money laundering hapo.
Huyu mwenye biashara alidai kuwa hana akaunti. Je, mwenye akaunti anawajibishwa vipi? Maana yeye aliitwa atoe akaunti yake itumike kwny kuingiza hela ya biashara, lakini kwenye makubaliano ya biashara hakuwepo, kumbuka aliitwa mwishoni
 
Alitakiwa kukataa kupitisha hela za mtu kwenye akaunti yake.

Mtu akikwambia hana akaunti mpe simu ya benki apige aulize akafungue akaunti.

Ukimpa akaunti yako wewe apitishe hela zake, hela zikiwa za biashara chafu unawajibishwa wewe na yeye.

Kutojua kosa si utetezi kisheria.
 
Alitakiwa kukataa kupitisha hela za mtu kwenye akaunti yake.

Mtuvakikwambia hana akaunti mpe simu ya benki akafungue akaunti.

Ukimpa akaunti yako wewe apitishe hela zake, hela zikiwa za biashara chafu unawajibishwa wewe na yeye.

Kutojua kosa si utetezi kisheria.
Sasa hapo anajinasuaje mwenye akaunti akihitaji kujitetea mkuu?
 
Anatakiwa kutafuta mwanasheria mzuri atakayejenga hoja kwamba huyu mwenye akaunti si mtu anayejua mambo haya kiundani na alidanganywa tu ili akaunti yake itumike bila yeye kuelewa biashara yenyewe ilivyokwenda.

Huyo mwanasheria aliyekuwepo katika hilo deal ni mwanasheria wa nani?

Akikutana na hakimu mzuri anaweza kupunguziwa adhabu au kuonywa.

Ila ukweli kwamba kachukua sehemu ya hela unamfanya aonekane kama alielewa kuna njama hapa akakubali kuingia deal kwa sababu alitaka hela. Ingekuwa rahisi zaidi kisema kadanganywa kama angekuwa hajaliowa hela.
 
Mwanasheria ni wa huyo muuza bidhaa
 
Mwanasheria ni wa huyo muuza bidhaa
Utetezi wako mwingine hapo ni kwamba wewe ulimuamini huyo mwanasheria in "bona fide" kwa roho nyeupe ukijua kwamba mwanasheria hawezi kukudanganya na amehakiki mambo kuwa yako sawa, lakini kwa kuwa mwanasheria ni wa huyo jamaa, wamepanga mpango kukudanganya wewe usiyejua sheria na wewe hukujua sheria na hukuwa na mwanasheria wako.

Hilo haliondoi kosa lako, lakini linaweza kuonyesha kwamba uliingizwa mkenge ukifikiri mwanasheria anapitia vitu kuhakiki uhalali lakini alitumika kukudanganya.

Hapo unapunguza kosa lako kutoka njama za money laundering kwenda ujinga wa kuamini watu sana.

Ujinga si utetezi, ila ni kitu ambacho hakimu anaweza kukusamehe au kukupunguzia adhabu.

Ila ukionekana umekula njama utapata matatizo sana.
 
Asante sana kwa msaada wako Mkuu... Inshallah Mwenyezi Mungu akuzidishie palipopungua
 
Asante. Lakini mimi siamini kwamba Mungu yupo.

Ndiyo maana nimekusaidia kukupa ushauri.

Ningeamini Mungu yupo nisingekupa ushauri wala contact.

Ningekwambia omba Mungu.

Kwa hiyo shukuru siamini kwamba Mungu yupo.
 
Umenitisha kdg Mkuu hapa
 
Asante. Lakini mimi siamini kwamba Mungu yupo.

Ndiyo maana nimekusaidia kukupa ushauri.

Ningeamini Mungu yupo nisingekupa ushauri wala contact.

Ningekwambia omba Mungu.

Kwa hiyo shukuru siamini kwamba Mungu yupo.
Hello my fellow learned brother.

Kwa hoja hiyo about God si sahihi. Mungu yupo na aliuumba huu ulimwengu kisha akampa akili na uwezo mwanadamu ili autawale. So haitakiwi kumuomba Mungu ili matatizo yako yaishe then umekaa. Anachotaka Mungu ww uchukue hatua kwa akili zako yy amuombe tu abariki hatua zako..

Mungu yupo, ila hizo dini ndio zinampumbaza Mwanadamu
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Unamuamini Mungu gani?
 
Back
Top Bottom