Msaada wa kisheria Juu ya huyu mtoto

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,625
1,619
Habari zenu wabobezi wa sheria!

Kuna kaka yangu fulani kwa sasa ni Askari, lakini wakati anaanza chuo alitembea na dada mmoja hivyo aka bahatika kumpatia mimba na sasa ana mtoto wa miaka 5.

Tangu kipindi hicho chote jamaa alikuwa anatoa huduma kama kawaida, sasa tangu mwaka jana jamaa akutaka tena kuwa na mahusiano na huyo mzazi mwenzake, hivyo basi akampa " go ahead " afanye mambo yake.

Sasa, Juzi huyo binti akamwambia kaka kuwa hakubali kupotezewa muda wake bure, kwa hiyo anataka fidia ya sh. Laki tano, ndipo amruhusu kaka kuendelea na maisha mengine.

Mama mtoto akazidi kwa kusema, anampa siku saba tu, vinginevyo atajua nini cha kumfanyia.

Swali: 1. Je, ni kweli binti ana haki kisheria kudai fidia ikiwa hawakufunga ndoa, na kama huduma kaka alikuwa anatoa

2. Huyu binti wakati fulani alikuwa anatoa lugha za vitisho sana, Je hili aliwezi kutumika kama ushahidi kumshitaki huyu binti??

3. Kama kaka akitaka mtoto wake, je taratibu kisheria zikoje?

4. Sheria za vyombo vya usalama zinataka mtu asiye na mtoto wakati anajiunga nao, Je kwa hili binti akienda kutoa taarifa ofisini kwa kaka hatma yake itakuwaje??

Ahsante, karibuni kwa ushauri.
 
Vitisho ni kosa la jinai. bro aende polisi kutoa ripot..

Turudi kwenye mada... Kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya tanzania mtoto chini ya miaka 7 anapaswa kuish na mama kwa kuangalia baadhi ya vigezo kama uwezo wa mama na mazingira ya ustaw wa mtoto... Kama mama hana mazingira mazur ya ustaw wa mtoto baba atapewa aishi na mtoto hata kama ana miaka miwili..

Suala la fidia... sion kama inawezekana kama jamaa alikuwa akimhudumia kila kitu mtoto wake...

Akiona anatatizwa sana mwambie kaka yako aende ofisi za ustaw wa jamii akaweke mambo sawa
 
Back
Top Bottom