Msaada wa kisheria, je nani anapaswa kulipa gharama kwenye hili la kiwanja?

Clemoo

Member
Nov 27, 2011
71
15
Habari za week end wakuu, naomba msaada nilitaka kufahamu, ikiwa unataka kununua kiwanja kwa maandishi ya serikali za mtaa, je anayetakiwa kulipia garama hizo ni mnunuzi au muuzaji wa kiwanja
na je garama hizo zikoje?
 
Habari za week end wakuu, naomba msaada nilitaka kufahamu, ikiwa unataka kununua kiwanja kwa maandishi ya serikali za mtaa, je anayetakiwa kulipia garama hizo ni mnunuzi au muuzaji wa kiwanja
na je garama hizo zikoje?
Kwakawaida muuzaji anatakiwa kulipia...ila imekuwa mazoea wote mnachangia.
 
From what I know muuzaj anachangia 50% pia mnunuzi 50% ya 10% ya gharama nzima ya kiwanja au thaman ya kiwanja
 
Kimsingi gharama ya kufanikisha mauziano ya kiwanja yanatakiwa kufanywa kwa watu wanaoruhusiwa kufanya kazi hiyo kisheria, kwa lugha halisi ni wanasheria au watu wanaojihusisha na uuzaji wa masuala ya uuzaji wa ardhi (conveyancers) ambao ni lazima wawe na leseni ili kufanya hizo kazi.. Lakini kwa vile gharama za hawa watu ni gharama sana basi wengi wet tumekua hatuwatumii hawa watu na badala yake tumekuwa tukiwatumia wajumbe wa serikali za mtaa (ambao wanafanya kazi hii kimakosa kisheria- hawana uhalali wa kufanya hivyo) kwani gharama zao zimekuwa ni za chini kuliko za hao conveyancers.. Ni kosa na hata wao (serikali za mtaa) wanajua na ndio maana hawatoi stakabadhi kwa malipo hayo
Tukija kwenye swali lako, jibu ni kuwa muuzaji ndiye anaetakiwa kutoa hiyo pesa (ambapo akiamua anaweza kuijumlisha kwenye gharama za ununuzi na hivyo ukaitoa wewe mnunuzi) lakini uzoefu unaonesha kuwa mnunuzi na muuzaji huwa wanachangia gharama hizo nusu kwa nusu
 
Back
Top Bottom