Msaada wa kisheria iwapo nitasimamishwa kazi

guojr

Member
Dec 4, 2015
62
95
Mimi ni mfanyakazi wa kampuni flani hapa Dsm na mkataba wangu wa kazi unaisha Desemba 2017.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba kampuni inampango wa ku outsource operations zake kwenye kampuni nyingine. Hivyo sisi wafanyakazi wengine tutapunguzwa au kuhamishiwa kampuni nyingine.

Swali kwa wanasheria, sheria inasemaje iwapo nitasimamishwa kazi iwapo mkataba bado haujaisha au kuhamishiwa kwa mwajiri mwingine? Je kuna fidia yoyote nitapata kutokana na kusitishiwa mkataba au kubadilishiwa mwajiri?
Natanguliza shukurani.
 
Kama mtahamishiwa kampuni nyingine kwa mshahara uleule au wa juu zaidi hakuna shida, na sheria inakulinda kupewa ajira kwenye hiyo kampuni nyingine kwanza kuliko asiyemuajiriwa

kama hakuna nafasi, basi muajiri anakupa full salary ya mwezi mmoja isiyonamakato yoyote ili ujipange wakati unatafuta ajira nyingine
 
Nilisikia kama unatakiwa ulipwe mshahara wa miezi iliyobakia sababu ameku terminate bila sababu za kisheria kami vile under performance, kufilisika nk...
 
mimi nakuomba kwanza kasome vizuri mkataba wako unasemaje kwakua hata huyo mwanasheria hawezi kukusaidia bila kuusoma mtakaba wako unasemaje, mikataba mingi ya hapa bongo inasema km mmojawapo atavunja mkataba anatoa mshahara wa mwezi mmoja au vinginevyo sasa cjui mkataba wako unasemaje.Waafrika tunakasumba ya kutosoma mikataba yetu ya ajira tunapopewa na yakija mambo km haya hua tunapata shida sana, anza na hio ila kwa nijuavyo lazima kuna fidia atakulipa kabla ya kuvunja mkataba au atakuhamishia kwenda hio kampuni mpya bila malipo ila atakufahamisha na unaweza kuta benefits zako zikabaki vile vile au zikapungua.
 
Back
Top Bottom