Alan Madiga
Member
- Apr 28, 2013
- 26
- 2
Pole kwa unayoyapitia naelewa unachokiongelea na naelewa maumivu uliyonayo.Pole kwa kuhusishwa na masuala ya kikubwa kabla ya umri wako.Njia pekee ya kuepuka hali hio ni kuwasamehe hao wabakaji na walawiti wa watoto kwani hawajui makosa yao.Naamini mtu kwenye akili timamu hawezi kutenda waloyatenda hao.Usitumie background yako ya maisha kujenga ufa kwenye mahusiano yako ya sasa.Kumbuka wewe ulikuwa muathirika na hukuwa na usemi juu ya maovu uloyapitia lakini sasa una sauti,unaweza kuitumia sauti hio.Njia mmojawapo ya kuepukana na adha hio ni kuongea na wahusika face to face ili wajue makosa yao na wasiyarudie tena na nakuahidi wataaibika sana na kufedheheka.Bila shaka walikuona mtoto na wakajua hutokuja kukumbuka haya ukubwani na hawakuwa na ujuzi wa athari gani wanazokupandilia lakini watoto wanakumbuka mengi mno.
Ukiwa kwenye mahusiano kuwa muwazi na uongelee kuhusu maisha yako ya awali ili mwenza wako apate uelewa juu ya yale uloyapitia.Mueleze kwamba upo emotional unstable,una low self-esteem,depression, upo anti-social kama matokeo ya matendo hayo.Akikukubali wewe kama ulivyo utajenga imani nae na inatasaidia kudumisha mahusiano yenu.
you can learn to love quite well!cha kufanya anza na tamhiliya za kifilipino,wasamehe waliokukosea,soma vitabu vya mahusiano,mapenzi na saikolojia!fanya hivyo na ulete feedback!
Alan najua unaamini katika Mungu mwambie ashughulike na mambo yako lakini jiachilie wewe kwanza kakangu! kwakusamehe na waangalie wanawake katika mtazamo chanya.
La kwanza na la muhimu mno ni kuikubali hiyo hali, na kuichukulia kuwa yalikuwa ni mapito halafu cha pili ni kusamehe na kuanza upya kumbuka hawa unaowaumiza sasa hawana chembe ya kosa bali ni wahanga wa jinsia
Vilevile kuna watu udogoni mwao walitendewa mabaya kuliko wewe, wao walilawitiwa na ndugu wa damu, halafu pia jifunze kuwa wewe lakini usiwe katili kuna mengi mazuri na wengi wazuri ambao hawapaswi kuwa wahanga wa matendo ya wengine
Kwa kuwafanyia ukatili unaendeleza ile roho kwakuwa wao walijitoa kwako kwa upendo mkuu lakini ukawaumiza nao wataenda kuumiza wengine
Samehe na uwaachilie waliokuumiza .
Nafsi zetu zina masikio na macho ongea na nafsi yako kwa kumaanisha kuwa umechoka kutumikishwa na roho za kisasi unataka kupenda kama ambavyo binadamu wengine wanavyopenda.
Najua utakuwa na vigezo vyako katika kumpenda mwanamke utampata na utenjoy.
Lakini kubwa kabisa ni kusamehe na kuwaachilia hao watu ulio washikilia
Mi nimechoka hali hii lakini hisia mbaya zinanikaba sana.
Duh! Ndugu usije ukawa unatumia kubakwa kwako kama sababu ya kuwaumiza watoto wa kike.Mimi sioni kama kubakwa kwako kunaweza kuwa na athari kiasi hicho kwako,watoto wa kike ndio huwa wanaathirika sana kwa hilo ila sio wa kiume,by the way ulikuwa mtoto na ulikuwa hujui kinachoendelea so inakuathiri vipi?
Nina marafiki zangu wawili ambao waliyajua mapenzi wakiwa wadogo kupitia kwa house girls na haijawahi kuwa athiri kiasi hicho.Sitaki kuamini kuwa wao ni tofauti sana na wewe kiasi kwamba wewe ikuathiri kiasi hicho.
Wewe hiyo chuki umeijenga kwa kupenda mwenyewe na ni tabia yako ya umalaya ndio inakufanya usipende not otherwise.Its not a psychological problem,acha umalaya chagua mmoja kati ya hao utulie naye.
Mimi naomba tuonane hapa si mahali pa kuweza kuongea kila kitu, kama uko tayari ningependa tuonane!
Kwanini unakuwa na mtazamo hasi kwanini unaamnini hakuna atakaye kuelewa ? Je ni kwasababu ya unawamistreat?Natamani sana kuwa na mahusiano lakini hakuna anayeweza kunielewa.