Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,939
Mkuu kuna mdogo wangu wa kike anasumbuliwa na Maruhani mno, moja ya matukio yanayomsumbuwa ni pamoja na muda mwingine kushindwa kupumua, au kupoteza nguvu au kuwa na hali ya kuyumbayumba kama mtu anayetaka kupandisha majini, anapenda sana kuwasha udi mno chumbani mwake, pia kuna muda akiamka anakuta amechanjanjwa chale, na kuna kipindi alibreed miezi mitatu none stop, pia kuna kipindi anaweza kukaa anaangalia darini bila kupepesa macho na wala akiitwa hawezi kusikia mpaka hali hiyo ya kuangalia huko juu iishe, pia kuna kipindi anaota akiwa amezungukwa na maiti au kuona maiti ikiamka na kwenda kujizika au muda mwingine akisikia kuna msiba anakuwa hajisikii amani yaani kifupi hawezi hudhuria msiba wowote. Kingine anachukia kuwa kwenye mahusiano yoyote na ikitokea mwanaume akijitikeza anabadirika mno.
Kifupi hali hii ilianza baada ya kufuata na Mwanaume mmoja kuhitaji kumuoa na yeye kukataa ndipo hali hiyo ikamuanza . Amefika sehemu anatamani aende kuombewa actually anaenda lakini baadae hayo madudu yanamzidi nguvu anasitisha muendelezo. Lakini kwa sasa amechoka anatamani hiyo hali imtoke awe binadamu wa kawaida.
Kuna kipindi akiingia nyumba yoyote huwa anabadirika miguu yake huanza kutetemeka na hali iliyotajwa hapo humtokea na akiondoka ndiyo hupata amani.
Naomba watalaamu na wale wajuzi msaada wenu kumsaidia huyu mdogo wetu Jamani.