ngosha2011
JF-Expert Member
- Aug 20, 2011
- 681
- 87
Mimi na mpenzi wote ni wafanyakazi kabla hatujaenda kwa wazazi kujitambulisha,imetokea mpenzi wangu kapata ujauzito,na anasema hayupo tayari kuzaa kwa sasa,sababu kubwa kwao ni mtoto wa kwanza na itakuwa aibu kuwa na mtoto kabla ya ndoa,analia kila muda na amani haipo kabisa,nashindwa nifanyeje na mimi sina tatizo kuhusu huo ujauzito,hapa nilipo nimetingwa,maana anasema ni bora anywe sumu tu afe,msaada ushauri wenu kwa hili tatizo
Uja uzito una mda gani? Kama ni mdogo ni bora mkapeleka mambo haraka sana,yani mkafanya taratibu za ndoa hata ya ki-serikali alafu mengine yakafuata.,Mnaweza msieleweke kwa watu lakini itakuwa bora kuliko hali ilivyo kwasasa!
Oa mara moja mkuu.........
Anajua uja uzito siyo wako. Kwani we siku ile hukuniona?
Kwani ndio amejua itakuwa vibaya kupata mimba kama mtoto wa kwanza kwenye familia baada ya kuwa na hiyo mimba au hata kabla alikuwa analitambua hilo? Kama alikuwa anatambua na akakushirikisha kwa kukwambia wewe ulimpa mrejesho gan?
Swala hapa kwa sasa sio wewe kutokuwa na tatizo na huo ujauzito, la msingi kwa sasa je uko tayar kufuata taratibu (ndoa) ili kunusuru uhai wa hao viumbe wawili?
Tahadhari: utoaji wa mimba usije kuwa ndio njia mkato ya kumaliza huo utata wenu manake wakati mnafanya kwichi kwichi mnlikuwa timamu na mlikuwa mnajua matokeo yake! Sasa ndo maji hayo ushayavulia nguo sharti uyaogee.
Hata mkifunga ndoa mtazaa, sasa kama aliyafahamu hayo kwanini hakutumia kinga? Au imani yake inaruhusu dhambi ya kutoa mimba?
kwanini hataki...?..ukizingatia kwa hali hiyo uwezi kataa mhusika akajitambulishe kwenu.....hataki na mimi nipo tayari na ujue tunaishi pamoja mpaka sasa
jitahidi uwezavyo......hiyo dhambi ya kutoa mimba uiepuke......baki na msimamo wako wa kwenda kwao ukajitambulishe....usitetereke.......mtoto raha sana......tafadhali msiukatishe uhai wa huyo mtoto......binafsi sababu zote anazosema huyo dada siyo za msingi.....hairuhusu ila analazimisha,mara tena anasema anaogopa hicho kitendo,tatizo anashinda analia tu
hataki na mimi nipo tayari na ujue tunaishi pamoja mpaka sasa
kwanini hataki...?..ukizingatia kwa hali hiyo uwezi kataa mhusika akajitambulishe kwenu.....
kama unaweza washirikishe wazazi wako wakupe mwangaza zaidi.....ila msisitizie huyo dada kuwa hauko tayari kutoa mimba......ata ikiwezekana mdanganye kuwa kimila kwenu mtu akitoa mimba lazima afe......au hatokaa apate mtoto maisha yake yote......au atakuwa kichaa ambacho hakitakuwa na tiba.....
hairuhusu ila analazimisha,mara tena anasema anaogopa hicho kitendo,tatizo anashinda analia tu
jitahidi uwezavyo......hiyo dhambi ya kutoa mimba uiepuke......baki na msimamo wako wa kwenda kwao ukajitambulishe....usitetereke.......mtoto raha sana......tafadhali msiukatishe uhai wa huyo mtoto......binafsi sababu zote anazosema huyo dada siyo za msingi.....
he makubwa poleee ngosha wa watu kwa yanayokukuta ndoa hataki,mimba bila ndoa anadai unamtia aibu kwao at the same time mnaishi kinyumba.Jamaniii wonders shall never end watu8 njoo uone makubwa mengine sasa huyo mama kijacho umemuuliza anataka nini ndo kakujibu anataka kujiua?
na kwa kuongezea hapo mwaka huu wengi wamefariki kwa kutoa mimba wengi sana naowajua au wengine wanatibua magonjwa especially VVU vilivyolala