Msaada wa haraka, mwanangu kameza kidude cha plastic

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
728
Waungwana mtoto wangu wa miaka 6 amemeza kidude vha plastic wakati anacheza kwa mujibu wa maelezo yake ila analalamika maumivu ya kifua anasema kimekwamia kifuani. Naomba mwenye kujua namna ya kumsaidia mtoto aliyemeza kitu ni kwamba hakijakwama ila inaonekana kimekwamia maeneo ya kifuani kwa kuwa analalamka maumivu kifuani nimejaribu kumnywesha maji ili kiteremke lakn meshindikana nimejaribu kummezesha matonge ya ugali lkn bado .
Naelekea hospotali ila naomba msaada wamawazo.
 
Weka picha tafadhali.Unamwacha mtoto anateseka kwa maumivu halafu unakuja JF.Ninyi ndo mnaopiga picha ajali zinapotokea badala ya kutoa msaada.
 
Mkuu muda huu ulio online ungekuwa umefika hospital ungekuwa ushapatiwa huduma.

Ushauri wangu hospital ni bora kwa afya kuliko jf

Btw pole sana
Laiti ungenisoma mstari wangu wa mwisho usingenishukia kiasi hicho nimeandika uzi huu nikiwa njiani kuelekea hospitali
 
Laiti ungenisoma mstari wangu wa mwisho usingenishukia kiasi hicho nimeandika uzi huu nikiwa njiani kuelekea hospitali
Kila la kheri mkuu usisahau kuleta mrejesho na kapicha fulani amaizing
 
Mkuu nashukuru ni kuwa dogo amepata huduma inaonekana hicho kidude kilishuka tumboni ila kilimwachia mikwaruzo kwenye njia ya chakula ndo maana alikuwa anasikia maumivu
Anaendelea vizuri
Thanks mkuu kwa mrejesho, Mungu amsimamie na kumpa afya njema
 
hapo sasa uwe makini kukagua nnya yake ili ujiridhishe kuwa kimetoka mana sidhani kama plastic itakua digested. Fuatilia mpaka ukione ulete mrejesho hapa hasa ukubwa wake ikiwezekana na kapicha
 
Mmh.mmoja aliweka kifuniko cha peni kile cha nyuma puani mmh ilikuwa hatari..
 
Back
Top Bottom