Msaada wa haraka: Kaka wa kwenye foleni

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
17,280
16,556
Siku moja nilikuwa na shoga yangu njiani tunaelekea Ilala boma kusagula viwalo

Shoga yangu akafunguka;
Eh bora nimekumbuka, kuna kaka nimetokea kumpenda sana, kila siku nikiwa naenda kazini asubuhi, nakutanaga nae kwenye foleni, kaka mzuri sana mzuri maji ya kunde classic flan amazing.

Nikaanza kum-noti, nanoti plate no, rangi ya gari, muda wa kukutana kwenye foleni kila siku nikawa nawahi nikutane nae tu, nasikia raha kumuona.
Ikawa hivyo, kwa muda wa miezi 6 nazidi kumpenda, yeye hajui wala nini, naumia tu moyoni.

Baada ya miezi 8 nikakutana nae akanipungia mkono, na mie nikajibu, ikawa tukikutana kila mtu kwenye gari lake, tunawashiana taa au kupungiana mikono yani vyovyote vile.

Siku 1 nikachelewa kutoka home, usingizi ulinoga, nikajua hapa nimeshakosa kumwona kaka mzuri, kufika ile sehemu tunayoonanaga kwenye foleni namwona amepaki pembeni anashuka, kumwangalia naona anatoa magongo anashusha miguuu, eh kumbe Mlemavu!
Nilichoka ghafla! Dah stimu ikanikata fasta!

Nikaondoka njia nzima nasononeka. Sijui nafanyaje, Kumpenda nampenda kumwambia nashindwa kila siku tukionana ni kupungiana tu

Money penny nisaidie, ila nimesikia walemavu ni watamu balaa hapa nazidi kuchanganyikiwa, kiukweli nampenda ila ile hali yake imenishtua kidogo, mimi nilikuwa nampatia picha nyingine kabisa.

Jamani mnamsaidiaje shoga yangu? Moyo ushapenda. Amwambie au auchune?


 
Mmh pole ndo hisia za maumbile ziko hvyo dada, kama una upendo ndani yako kwake ulio dhahiri ktk dhati mwambie tu

Lkn isije ikawa tale mambo mko ktk mahusiano mara unamletea malingo na nyodo za ,,, kwanza ww mlemavu,, utamkosea Mungu
Kama una mpenda jitoe kufa na kuzikana na mara nying watu hao usifanye utani nao maana Mungu yuko nao pamoja
 
Nimekumbuka tu huu mwimbo

Dah we mwana umenikumbushs mbali mpaka natokwa na mchozi
Doh!

Mmh pole ndo hisia za maumbile ziko hvyo dada, kama una upendo ndani yako kwake ulio dhahiri ktk dhati mwambie tu

Lkn isije ikawa tale mambo mko ktk mahusiano mara unamletea malingo na nyodo za ,,, kwanza ww mlemavu,, utamkosea Mungu
Kama una mpenda jitoe kufa na kuzikana na mara nying watu hao usifanye utani nao maana Mungu yuko nao pamoja
Kwakweli, Amina.

kwani ana ulemavu wa mshedede??
miguu amwekee ya bandia
Du! Aya boss

Mje na huku

Msaada wa fasta: Urasimu na Maendeleo
 
Back
Top Bottom