Msaada wa deni la trafiki makosa barabarani

Msaada wa deni la trafiki makosa barabarani

ikhufa

Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
33
Reaction score
21
Salaam,

Habari za mida hii wadau, bila kupoteza muda naomba niingie moja kwa moja kwenye mada, ilikuwa wiki kama nne zimepita nilipopigwa cheti barabara ya morogoro karibu na kimara kwa kosa la matumizi mabovu ya barabara na ilikuwa asubuh nikiwa najaribu kuwahi kazini na traffic alienikamata hakuwa na mashine ya kuniandikia hivo akaandika no ya leseni na gari kwenye kitabu chake na kuniambia kosa moja litasoma kwenye leseni yangu.

Basi siku zikapita nikijua muda wa kulipa deni ninao kama wiki hivi basi mishe zikaendelea, kwa bahat mbaya tena nikaandikiwa the same week kwa kosa jengine nkaona isiwe kesi basi nkaenda kwa wakala kulipa deni langu nkijua nina makosa mawili ila kabla ya kulipa nikamuomba wakala aniangalizie deni langu na akaniambia kuwa ni elfu 30. Nikashangaa kidogo lkn nkasema anyway huenda alisahau kuandika yule wa kosa la kwanza. Nkalipa 30k na nikaendelea na mishe zangu.

Siku, saa na dk zikapita kama baada ya wk 3 hivi maeneo ya bandari nikatanua njia kuwahi hosp wazee wa kazi hawa hapa nkapigwa cheti chengine duuh. Na siku hiyo hiyo nikiwa na mishe zangu maeneo ya ununio njiani nikasimamishwa na trafik nikaambiwa wanakagua madeni na nikatutwa nadaiwa 80k. Kwanza nikashangaa nikamwambia afande mbona leo ndo nimeandikiwa 30k hiyo nyengine inatoka wapi. Akasema yy hajui na napaswa kulipa deni.

Basi siku ya jana nkapita kwa wakala kwa lengo la kulipa deni nikiamini kwamba naenda kulipa deni lote 80k. Nkamwambia kama kawaida wakala aniangalizie deni. Akaniambia nadaiwa 60k. Hapo nikachoka kabisa from 80k to 60k. Nkalipa 60k the nkamuambia embu niangalizie tena kaniambia sina deni baada ya kulipa hiyo 60k.

Nb mpk sasa sina amani maana sijajua deni langu ni kiasi gani na najua kama ndaiwa huenda deni linaendelea kukua.

Je, nifanyaje niweze kumalizana na hawa jamaa.?

Nimejaribu kutumia link flani nlipewa na jamaa yangu lkn haikubali.

Msaada wakuu.. Wa mawazo
 
Huna amani na deni la week 2?
Nilipigwa fine mwaka jana mwezi wa sita kwa kosa la uonevu uliopitiliza.
Sijalipa lile deni hadi leo na barabarani natembea kama kawaida.
Sijui hilo deni limefika kiasi gani ila sitalilipa kabisa.
 
Ngoja nikupostie madeni yani hayo tuu unalia lia hivi, hapo nilikamatwa nikapunguza matatu 180k yanaanzia 2016
IMG_1890.JPG
 
Mkuu, inaonekana hufuati sheria za barabara
mkuu nafuata sheria vizur. makosa matatu kati ya manne ni wao trafik wamesbbisha wana turuhusu kutanua then unakutana na wengine mbele wanakupiga cheti
 
mkuu nafuata sheria vizur. makosa matatu kati ya manne ni wao trafik wamesbbisha wana turuhusu kutanua then unakutana na wengine mbele wanakupiga cheti

Pole sana kiongozi, Hawa OMBA OMBA nawajuwa vizuri ni waroho sana kwa pesa,
 
Yule police wa kwanza si namba na leseni anavyo mpaka sasa katika kalatasi lake. Akikosa kufikisha target anakwandikia tena na tena ili mambo yake yaende town hapa
 
Back
Top Bottom