Msaada: Vodacom na jaribio lao la kutaka kunitapeli

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,780
2,555
Wakuu nimenunua vocha ya elfu moja wiki iliyopita nikawa naiingiza kwenye simu yangu jibu nililokuwa napewa ni hivi"Samahani, kadi hii haipo tayari kwa matumizi kwa sasa,wasiliana na vodacom huduma kwa wateja namba 100"

Nikaamua niwapigie simu wakaniahidi kulishughulikia tatizo langu ndani ya masaa 24.Nimesubiri baada ya masaa 24 nikajaribu tena kuiingiza majibu ndo yaleyale kuwa haipo tayari.

Nimesubiri wiki nzima imepita na leo tena nimeingiza majibu ni yaleyale nikaamua tena kuwapigia vodacom na walichoniambia kuwa hiyo card number ya vocha kweli ni valid na system yao inaitambua but imeingia mtaani kimakosa na dealer aliyeichukua kwao na kuiingiza mtaani hawajamtambua so hawawezi kuwasilina naye eti niirudishe duka nililonunua ili nipewe either vocha nyingine or nirudishiwe pesa yangu.

Sasa hapo ndo nilipoona vodacom ni matapeli wawazi kabisa yaani one week imepita alafu nimrudishie mwenye duka vocha anaweza kunielewa kweli...afu siku niliponunua hiyo vocha nilikuwa safarini kwa hiyo eti mi nifunge safari kutoka hapa nilipo nisafiri kuirudisha vocha sehemu niliyonunua.

Vodacom huu mnaoufanya hauna tofauti na utapeli wa wazi kabisa na hautawafikisha popote na nitahakikisha tunafikishana mbali sababu ni uzembe wenuwenyewe katika kutoa huduma kwa wateja.

Voucher card number ni 0070901151 ila sijamalizia number mbili za mwisho kutokana na sababu za kiusalama.
 
halafu nashangaa wanapigwa fine milioni 27 tcra wanajisifu huku wanatuibia mabilioni kama iliingizwa kimakosa ni kosa la nani
 
Mleta mada nimependa sana msimamo wako katika kutafuta haki yako na wengine walio katika hatari ya kupoteza haki yao. Umenikumbusha ile habari kwamba Tanzania hii kuna watu wa kabila fulani wako tayari kuuza hata ng'ombe ili kupata fedha ya kuendeshea kesi ya kudhurumiwa kuku wao. Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa gharama yoyote.
 
Mkuu mitandao mingi ya simu imekuwa ikitufanyia utapeli wateja.huwa nasikia tu but sijawahi kuwa na ushahidi wa hili jambo ila kwa hichi wanachonifanyia vodacom ndo nimeamini kuwa hawa ni matapeli kabisa tena waliobobea
 
Mleta mada nimependa sana msimamo wako katika kutafuta haki yako na wengine walio katika hatari ya kupoteza haki yao. Umenikumbusha ile habari kwamba Tanzania hii kuna watu wa kabila fulani wako tayari kuuza hata ng'ombe ili kupata fedha ya kuendeshea kesi ya kudhurumiwa kuku wao. Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa gharama yoyote.
Mkuu nitahakikisha haki yangu haipotei kwa gharama yoyote ile.hakuna sehemu ambayo wizi wa wazi kabisa kama huu unakubalika
 
Ni vizuri kukomaa nao kwani inawezekana wateja wengi wanaibiwa na kupata usumbufu wa aina hiyo. Hili ni jambo ambalo wao wenyewe kama Vodacom ndiyo walitakiwa walidhibiti lakini kutokana na uzembe wao wateja wanapata usumbufu mkubwa pamoja na kupoteza fedha zao za kununulia hizo vocha wanazodai kuingizwa mtaani kimakosa.
 
Hizo vocha magumashi inawezekana kuna mtu kaanzisha kijikiwanda chake kichochoroni kampuni ziwe macho sasa hivi ni kazi tu
 
taja namba yako nikurushie voda ya buku mkuu nikufute machungu
 
Nimesubiri wiki nzima imepita na leo tena nimeingiza majibu ni yaleyale nikaamua tena kuwapigia vodacom na walichoniambia kuwa hiyo card number ya vocha kweli ni valid na system yao inaitambua but imeingia mtaani kimakosa na dealer aliyeichukua kwao na kuiingiza mtaani hawajamtambua so hawawezi kuwasilina naye eti niirudishe duka nililonunua ili nipewe either vocha nyingine or nirudishiwe pesa yangu.

Sasa hapo ndo nilipoona vodacom ni matapeli wawazi kabisa yaani one week imepita alafu nimrudishie mwenye duka vocha anaweza kunielewa kweli...afu siku niliponunua hiyo vocha nilikuwa safarini kwa hiyo eti mi nifunge safari kutoka hapa nilipo nisafiri kuirudisha vocha sehemu niliyonunua.

Vodacom ni problematic sana, hivi kwa akili zao kama hiyo vocha ulinunua Chalinze wakati unakwenda Tanga, wanakutaka urudi hadi Chalinze kwa vocha ya book?

Kadhalika kama vocha hazikuwa zimeingia sokoni basi wao waliibiwa, na wewe ndiye wangekutumia kuwasaidia kumkamata mwizi wao lakini hawajaona hiyo kama ni kasha kwao kwa kutokukupa ushirikiano mteja wao, it is as if wameshirikiana na mwizi kukuuzia mbuzi kwenye kiroba

Halafu huu uonezi wanaufanya kwa low income earners (basing on the price you paid) nakumbuka niliwaandikia malalamiko yangu hawajajitokeza kujibu, binafsi nawachukia and my family members have opted for Zain now
 
Hizo vocha magumashi inawezekana kuna mtu kaanzisha kijikiwanda chake kichochoroni kampuni ziwe macho sasa hivi ni kazi tu
Mkuu waliniambia niwatajie voucher card number nikawatajia na wakadai wanaitambua so ni valid na ipo kwenye system yao
 
Vodacom ni problematic sana, hivi kwa akili zao kama hiyo vocha ulinunua Chalinze wakati unakwenda Tanga, wanakutaka urudi hadi Chalinze kwa vocha ya book?

Kadhalika kama vocha hazikuwa zimeingia sokoni basi wao waliibiwa, na wewe ndiye wangekutumia kuwasaidia kumkamata mwizi wao lakini hawajaona hiyo kama ni kasha kwao kwa kutokukupa ushirikiano mteja wao, it is as if wameshirikiana na mwizi kukuuzia mbuzi kwenye kiroba

Halafu huu uonezi wanaufanya kwa low income earners (basing on the price you paid) nakumbuka niliwaandikia malalamiko yangu hawajajitokeza kujibu, binafsi nawachukia and my family members have opted for Zain now
Mkuu vocha zingekuwa zimeibiwa wangeniambia, so inavyoonesha hii ni njia ambayo wameamua kututapeli sisi wateja wao wakijua hatuna sauti ya kuusema huu wizi wao wa mchana kwepe
 
Hawa voda ni wezi kila Idara ..Jana nimejiunga na kifurushi cha wiki ili nipate gb 1 lakin cha ajabu baada ya kupata verification SMS ..withing minute nikapokea tena SMS kuwa salio lako limekwisha..just imagine 4000 ikawa imeteketea hewan!!wizi wizi tena wa wazi
 
Mkuu waliniambia niwatajie voucher card number nikawatajia na wakadai wanaitambua so ni valid na ipo kwenye system yao
Hiyo sio kesi mwizi hawezi kubuni mbali na bidhaa bandia hzo card number zikiwa 12 basi ninasoma kwenye system ila itatoa jina kuwa de -activate maana haipo au haijapelekwa sokoni bado ila pole sana
 
Hawa voda ni wezi kila Idara ..Jana nimejiunga na kifurushi cha wiki ili nipate gb 1 lakin cha ajabu baada ya kupata verification SMS ..withing minute nikapokea tena SMS kuwa salio lako limekwisha..just imagine 4000 ikawa imeteketea hewan!!wizi wizi tena wa wazi
Ukiwa na smartphone usijaze vocha kabla hujazima data hilo ni angalizo muhimu sana
Ingawa kwa voda inakula pesa nyingi kwa dakika chache mnoo
 
Hiyo sio kesi mwizi hawezi kubuni mbali na bidhaa bandia hzo card number zikiwa 12 basi ninasoma kwenye system ila itatoa jina kuwa de -activate maana haipo au haijapelekwa sokoni bado ila pole sana
Ahsante sana mkuu.hili jambo nitalifuatilia mpaka nione mwisho wake unakuwaje
 
Back
Top Bottom