Habari wapendwa, kuna kiusafiri aina ya toyota VITS new model chenye ingine ya piston 3 , kinashida ifuatayo:-
Ukipanda mlima kinapoteza nguvu na kuwa kama kina kwikwi, kama kina taka kuzima
ukisimama kwenye mataa yaani kipo kwenye D (drive) na mguu kwenye brake kina kuwa kama kinataka kuzima
Kina toa mlio kama wa miss!!
Tumebadili plug, tumebadili pump, tatizo limepungua ila bado lipo!!
Tatizo lilianza baada ya kutoka sheli moja hiv sito itaja kwa sasa!!
Nifanyeje kusolve hii ishu?