Msaada: Utajuaje kama mtu upo katika mahusiano sahihi au sio sahihi pale unapokuwa mchumba au mpenzi?

Hakuna binadamu mkamilifu. Ukiweza kumudu kuvumiliana kwa yale ambayo kila mmoja anaona ni mapungufu kwa mwenzi wake hewala
 
Mahusiano yana mambo mengi sana ila kwa

Mwanaume ili ujue nipo katika mahusiano sahihi au sio sahihi jifanye umeyumba kimaisha takribani miezi mitatu uone mtoto wa kike atakuvumilia au hawezi kukuvumilia

Kwa mwanamke mnyime mwanaume papuchi
 
Swali la kijinga..hivi wewe unashindwa kujua kitu sahihi kwako. Any ways nitakusaidia. Ni lazima uwe na vigezo, japo siyo lazima utakaye kuwa naye awe na vigezo vyote ulivyo navyo. Huwezi kupima uzuri wa kitu bila kuwa na vigezo. Pamoja na vigezo vingine kuna mambo ya ujumla ambayo utayaangalia kama ifuatavyo.

1. Je unafurahia mahusiano yako...kama hufurahii basi hauko katika mahusiano sahihi.
2. Bila shaka mnakaa mnaongea mipango ya muda mfupi na muda mrefu..mna badilishana maono etc..je mna maono yanayo endana? Unadhani anaweza kuwa mke/mme bora kwako.
3. Kuna vitu vyovyote vidogo vidogo ambavyo hupendi kutoka kwake...e.g. tabia ya uongo, kuchelewa appointment etc. Je unadhani unaweza ukavivumilia, je mmewahi kuviongea na nini mtazamo wake, je yuko tayari kurekebishika.
4. Anakupa msaada wakati unahitaji..siyo lazima fedha..shida yako anaifanya shida yake..
5. Anaupendo wa dhati juu yako...hii inapimwa kwa namba 4, lakini pia mienendo yake juu yako. Ni juu yako kufanya uchambuzi na kupima.

Mambo ni mengi ila.mwisho wa siku ni wewe na yeye ndo mnajuana.
 
Ni kama nyumba
Unapenda chagua nyumba ya kupanga..
Zipo nyumba unaziona na unasema aah ndo naitaka..na zipo zingine nzuri lakini roho inasita kabisa..

Ukiona kuna mtu roho inasita kabisa..basi ujue sio
 
Ivi mtu utajuaje kama hapa nilipo nipo katika mahusiano sahihi au sio sahihi hapa nilipo ili mtu ujitambue mapema

Hebu tusadieni katika hilii
Dalili kuu ya kwanza ukiwa kwenye mahusiano na ghafla ukaanza kujiuliza maswali ya namna hiyo basi moja kwa moja mahusiano uliyopo sio sahihi.
 
Ukiona moyo wako hauna amani na mpenzi wako tambua hauko ktk mahusiano sahihi

Ukiona kila siku wewe ndio unakuwa wa kwanza kumsalimia mpenzi wako kumjulia hali ujue haupo ktk mahusiano sahihi

Ukiona mpenzi wako yupo online whatspp anaweka status zaidi ya nusu saa lakini hajakupa hajakujulia hali ujue haupo sehemu sahihi

Ukiona mpenzi wako ana tabia ya kukumbushia vitu ulivyowahi kumkosea wakati mlishasameana ujue haupo mahali sahihi

Ukiona mpenzi wako yupo bize sana na mambo yake kiasi kwamba wewe kwake hata usipomtafuta halalamiki

Sasa ili uweze kuvuka hatua hii na ujitoe hakikisha una plan B anayekuweka keep bize na furaha yako yote ielekezee ukooo
 
Kama wewe mwenyewe ni mkweli katika mahusiano, utajua mapema tu kama mwenzako ni mtu sahihi
 
It depends ila determinant namba moja ni furaha. Tumeumbwa ili tuishi kwa amani na furaha.

Kama ulipo huna furaha napo jifanyie assessment kisha ongea na mwezio uone anamtazamo gani kuhusu hilo. How he/she responds itakupa mwangaza.
 
Back
Top Bottom