Msaada/ushauri kuhusu Mkopo wa Halmashauri

Sumu ya nyigu

Member
Joined
May 18, 2019
Posts
60
Reaction score
111
Kitaaluma Mimi ni Daktari wa mifugo, vet. kulingana na changamoto za mtaji ili niweze kujiajiri nafkiria kuomba mkopo halmashauri Kama million 5 hivi, kwa ajili ya kilimo na ufugaji, vitu gani vya msingi napaswa kuvizingatia ili kuongeza uwezekano wa kuupata? Naomba ushauri wenu juu ya hili, au kama Kuna ushauri m'badala ili niweze kutimiza Lengo tajwa.

Ahsante.
 
Wanakopesha vikundi tu. Unda kikundi Cha watu 5 au zaidi na muandae katiba ya hicho kikundi na andiko la mradi( mchanganuo wa mradi ukiwa mzuri, halmashauri watashawishika kuwapa pesa nyingi) na akaunti ya benki yenye jina la kikundi mlichounda.
 
Kwanini uumize kichwa kwakufikiri wakati benki zipo
 
Wanakopesha vikundi tu. Unda kikundi Cha watu 5 au zaidi na muandae katiba ya hicho kikundi na andiko la mradi( mchanganuo wa mradi ukiwa mzuri, halmashauri watashawishika kuwapa pesa nyingi) na akaunti ya benki yenye jina la kikundi mlichounda.
Kwa andiko la mchanganuo au mpango wa biashara tuwasiliane(business plan)pm tafadhali
 
Kitaaluma Mimi ni Daktari wa mifugo, vet. kulingana na changamoto za mtaji ili niweze kujiajiri nafkiria kuomba mkopo halmashauri Kama million 5 hivi, kwa ajili ya kilimo na ufugaji, vitu gani vya msingi napaswa kuvizingatia ili kuongeza uwezekano wa kuupata? Naomba ushauri wenu juu ya hili, au kama Kuna ushauri m'badala ili niweze kutimiza Lengo tajwa.

Ahsante.

1. Hakikisha mnaunda kikundi kuanzia watu watano (umri miaka 18 usizidi miaka 35)
2.Andaa picha passport size ya kila mwana kikundi
3.Andaeni katiba ya kikundi
4. Andaa andiko la mradi (hakikisha unaonesha mchanganuo wa bajeti yenu mnayoomba mfano hiyo milion 5 mtafanyia nini)
5. Nendeni ofisi ya kata utakuta afisa maendeo ya jamii atakupa fomu mtajaza taarifa za wanakikundi kisha kuna sehemu afisa maendeleo au mtendaji ata saini
6. Utaenda halmashauri/manispaa Kwenye ofisi za maendeleo ya jamii (wao wanahusika na kuchakata maombi na kutoa mkopo)
7. KAMA kikundi chenu hakijasajiliwa basi mtapewa namba ya malipo mtalipa kiasi nadhani ni 5000 watasajili (lazima usajili kikundi ili maombi yafanyiwe kazi)
8. Maombi yenu yatapokelewa na afisa maendeeleo halmashauri kisha utapiga copy cheti cha kikundi kuonyesha kikundii kimesajiliwa na pia utapiga copy zile fomu za maombi
9. Ukishapiga copy submit hizo copy ofisi ya kata kwa afisa maendeleo kata

Ikumbukwe waombaji ni wengi na wenda bajeti ni ndogo haitoshi kwaivyo unaweza usipate mkopo kwa wakati ila muhimu ni kuandaa andiko zuri la mradi linalovutia na kushawishi ili upate nafasi

Mkopo wa vijana na wakina mama inatolewa katika vikundi kuanzia watu watano na kuendelea isipokuwa mikopo wa watu wenye ulemavu hii hutolewa kwa vikundi au mtu mmoja mmoja.

Mengine wadau wataongezea.
 
This one exhausted everything, thank you .
 
Back
Top Bottom