Msaada; upatikanaji wa vyeti chuo kikuu

Kiziwanda chema

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
291
477
Salaam wakuu
Natumai ni wazima na poleni na pilika za maisha na masomo
Kuna tatizo moja limenikuta siku ya jana nilipofika chuoni (University) kufuata cheti.

Kiufupi ni kwamba graduation ya chuo ilishafanyika tangia mwishoni mwa mwaka ulopita na sikuweza kutokea kweny list ya wahitimu kutokana na financial reason ambayo nimei-clear jumatatu ya wiki hii.

Sasa baada ya kufanikisha clearance shida ipo kweny suala la kupewa cheti. Wanadai siwezi kupewa cheti kwa sababu sikutokea kweny list ya wahitimu, hivyo natakiwa nisubiri graduation nyingne ndipo nipewe cheti. Na sababu kuu ni hiyo tu hamna nyingne.
Cheti kipo tayar ila siwez kupewa for only that reason.

Nimejiuliza maswali mengi ila nimekosa majib sasa wakuu labda mnisaidie kimawazo na vip kuhus hili wako sahihi?

Kila nikiwaza nakosa jibu maana mwaka mzima bila cheti dah !!!
Au nini kifanyike ili nipewe cheti
Msaada tafadhali
 
Mm ninachojua km upo kwenye graduation book maana yake upo clear kwa kupewa cheti hata km hukufika kwenye graduation siku hyo

Km haupo kwenye graduation book maana yake bado una mgogoro wowote na chuo

Km unadai hadi cheti kipo basi hiyo ni upuuzi wa hao wahusika
 
Pole sana. Taratibu huwa zipo hivyo.

Kwa busara tu, Fanya Mpango Uongee na Mkuu wa Chuo umueleze shida yako. Kama cheti kipo na shida ni Graduation list, basi muombe akupe cheti kisha jina lako litokee tu kwenye List ya Mwaka unaokuja.

Hata hivyo cheti chako ni cha mwaka huo hata kama haupo kwenye List.
 
Pole sana. Taratibu huwa zipo hivyo.

Kwa busara tu, Fanya Mpango Uongee na Mkuu wa Chuo umueleze shida yako. Kama cheti kipo na shida ni Graduation list, basi muombe akupe cheti kisha jina lako litokee tu kwenye List ya Mwaka unaokuja.

Hata hivyo cheti chako ni cha mwaka huo hata kama haupo kwenye List.
Asante kwa ushauri mkuu
 
Bado hujagraduate wewe, umemaliz malipo sawa, sasa subiri next graduation, ndio utapewa. Ni utaratibu hata wala usihamaki
 
Back
Top Bottom