Msaada: Ujauzito wa wiki 41 na hakuna uchungu

Msaada: Ujauzito wa wiki 41 na hakuna uchungu

Jamani msaada!nina ndugu yangu ni mjamzito wa mtoto wake wa pili Kwasasa una muda wa wiki 41 ndio imeanza!

Mimba yake ya kwanza alijifungua kawaida katika wiki ya 37 salama kabisa!sasa ujauzito huu wapili umemsumbua saaana mpaka leo hii hajajifungua na hakuna dalili!

Tarehe ya makadilio kwenye kadi iliandikwa tarehe 17/07 na baada ya Ultrasound ilisoma atajifungua tarehe 27/07 ila mpaka leo bado bilabila!mama amechoka saana!!!hospt wamemwambia asubiri mpaka tarehe 29/7 ndipo arudi tena watajua cha kufanya!![emoji17]

Msaada kwa aliyepitia changamoto hii alifanyaje

Pole kwa sintofahamu mtoa mada. Lakini zingatia:

1: Mtoa post namba mbili.

2: Huyu mama ndo ameanza wiki ya 41, mwache aimalize hizo wiki pamoja na siku 3.

3: Maamuzi ya hili hutegemea na uhakika wa taarifa alizozitoa mama mjamzito, hesabu sahihi na yale yanayoonwa na matabibu wakati wa kliniki mfano: kimo cha mimba nk.

4: Hivyo, kama hutakuwa umelidhika na mwenendo mzima basi ni muhimu kukaa chini na daktari bingwa mwingine na kukokotoa yote, kuangalia mwenendo wa ujauzito wakati wa kliniki na kumwangalia mama mjamzito kuhakiki yanayoendelea.

Ultrasound ni suppliment tu kwenye wiki kuanzia ya 36 kuhusiana na umri wa ujauzito. Itakupa taarifa nyingine kwa usahihi zaidi kuliko umri na INATEGEMEA NA MFANYAJI ULTRASOUND/KUTAFSIRI PIA(COMPETENCE).
 
Umeambiwa UTSS imesoma tarehe 27 na haijafika ila ushaanza kubwabwaja.!!
 
Hapanaa usiridhike nenda Hospital nyinginee aisee unaweza kumkosaa mtoto...!! Tusiishi kwa mazoeaaa...
Rikiboy unazingua...

Wapishi wengi huharibu mchuzi..

As long as mtoto anacheza, uss imeonesha yuko.vizuri, ameshageuka, basi hamna haja ya kuwa na wenge..

Kwanza inawezekana huyo mama hajui alishika mimba lini, na uss huwa inakadiria tuu haitoi exactly date of conception, usikute hapo alipo mimba ina wiki 35...

Akae kwa kutulia tuu, as long as mtoto anacheza basi hakuna kilichoharibika.
 
Rikiboy unazingua...

Wapishi wengi huharibu mchuzi..

As long as mtoto anacheza, uss imeonesha yuko.vizuri, ameshageuka, basi hamna haja ya kuwa na wenge..

Kwanza inawezekana huyo mama hajui alishika mimba lini, na uss huwa inakadiria tuu haitoi exactly date of conception, usikute hapo alipo mimba ina wiki 35...

Akae kwa kutulia tuu, as long as mtoto anacheza basi hakuna kilichoharibika.
mkuu kweli ultrasound inaweza kosea kukadiria siku ila not to that extent pia ultrasound haiitaji kujua conception date kufanya right apprximation... ila all in all inategmea kaenda hospital gani trust me.
 
Ni kweli, mpaka wiki ya 42 bado ipo ndani ya muda sahihi. Ikizidi hapo then ndio watai-term kama postdate.

Pia kwa research zilizofanywa na wenzetu inaaminika kuwa watoto wanaochelewa kuzaliwa wanakuwa na uwezo mkubwa wa akili.

Vuta subira kidogo.
Mmmh thanx mkuu kwa haya maelezo...japo ni utachoka mpaka ukomee[emoji26]
 
yeah japo ni wachache hufika huko, s unajua hua mimba inahesabiwa kwa wiki na sio mwezi mana kila wiki kunakua na mabadiliko kwamtoto wengine hujifungua kuanzia wiki 36, wiki 38, wiki 40 na had hukoo wiki42 yan ikifika hio 42 uchungu haujaanza automatic watakuanzishia tu
Sawa kipenzi ....nakumbuka ule uzi wako ulikuwa mama k, nilikuwa nakufatilia sana
 
Jamani msaada!

Nina ndugu yangu ni mjamzito wa mtoto wake wa pili Kwasasa una muda wa wiki 41 ndio imeanza.

Mimba yake ya kwanza alijifungua kawaida katika wiki ya 37 salama kabisa!sasa ujauzito huu wa pili umemsumbua saaana mpaka leo hii hajajifungua na hakuna dalili.

Tarehe ya makadilio kwenye kadi iliandikwa tarehe 17/07 na baada ya Ultrasound ilisoma atajifungua tarehe 27/07 ila mpaka leo bado bilabila! Mama amechoka saana. Hospitali wamemwambia asubiri mpaka tarehe 29/7 ndipo arudi tena watajua cha kufanya!![emoji17]

Msaada kwa aliyepitia changamoto hii alifanyaje.
Yawezekana mama hajui siku yake ya mwisho kuanza kuziona ck zake

USS inapigwa miezi 3 ya awali ndiyo inakuwa na uwezo wa kubaini vzr zaidi ya hapo haiwezi kusoma vzr

Ikifikisha wiki ya 42 lazima ajifungue kivyovyote vile mpeleke hosp wiki ya 41+6

Sawa mkubwa
 
Back
Top Bottom