Msaada: Tutoeni ushamba mimi na mke wangu

Msaada: Tutoeni ushamba mimi na mke wangu

Katafute passport na mkeo kisha mkapate chanjo ya homa ya manjano pale hospitali ya mnazi mmoja. Baada ya hapo unaweza kwenda ubalozi wa SA kupata maelezo ingawa SA watanzania hatuendi na viza ila muhimu kwenda ubalozini wakupe maelekezo ya nn kinahitajika kwa kuwa wewe bado ni mgeni. Kuhusu kupanda ndege nashauri ujifunze kupitia youtube kuna watu wengi wameweka video jinsi gani ya ku check in na kucheck out utapata mpka za Oliver Tambo Airport.

Cha muhimu kuwa mpole soma mchezo ukoje kwa JNIA wala hutopata shida wafuate tu abiria wenzako wanachofanya nawe iga. Kwenye ukaguzi utatakuwa kuvua viatu, mkanda, toa wallet na coins ndio utapita bila bugudha.

Siku ya kurudi pale Oliver Tambo inaweza kuwa shughuli maana ni airport kubwa na ina terminal nyingi ukiona unashindwa kuelewa uliza askari au wafanyakazi wa airport maulizo watakuelekeza vizuri sana.

Usisahau kubeba hela ya shopping kidogo
 
Heshima kwenu wakubwa zangu wa jukwaa hili na marahaba kwa wale wote niliowatangulia kuliona jua.

Mimi na mke wangu tumefunga ndoa takatifu wiki moja iliyopita, hivyo tukapanga tukatembee nchini Afrika Kusini.

Maana tangu kuzaliwa kwetu hatujawahi fika katika nchi hiyo na sio siri wote tunahamu ya kwenda kutoa ushamba.

Ifahamike kwamba sio mimi wala mke wangu aliyewahi kupanda ndege tangu kuzaliwa kwetu. Nahitaji kuelekezwa taratibu za ukataji tiketi, kupata passport ya kusafiria na namna ya kuingia airport kupanda chombo kuelekea South Afrika. Ili tusionekane washamba wa mambo ya kidigital.

Nb: Afrika Kusini nina ndugu, jamaa na marafiki wengi wanaishi huko, hivyo sehemu yakufikia sio shida.

Nawasilisha kwenu.
Kwanza Tafuta Passport ,Ingia fastjet kata tiketi panda ndege. Huitaji viza kwenda South Africa
 
Mkifika iringa husisahau kushuka hotelini kitonga mpate chakula cha mchana alafu ndo muendelee na safari yenu ya south Africa
 
Nenda ofisi za uhamiaji mahali ulipo Jaza fomu na uambatanishe yote yanayohitajika ili mpate passport,baada ya hapo nenda ofisi za ndege utakayopenda kusafiri nayo ili upate tiketi zenu. Mambo mengine utayajua tu ukiwa safarini
Mkuu ndio nilitaka kumwambia hivyo.

akishapata Passport ajue South hana haja ya kuomba visa.
yeye ajiendee zake FastJet au SA akate tiketi ila ajue atakaa siku ngapi ili asije kata tiketi mara mbili
 
Kutembelea Afrika kusini wakati hujawahi kupanda mlima kilimanjaro au kutembelea mbuga ya wanyama ya ngorongoro ni uwendawazimu!
 
wewe umeoa jana yamkini hata nyumba huna unataka kwenda A. Kusini, tena kuwatembelea tu jamaa na marafki, ushaur wangu acha kushadadia maisha fanya vitu vya maana kwanza starehe badae. Yangu hayo tu.
 
Safiri i local kwanza wakati unafanya mchakato wa passport.ingia website ya uhamiaji utapata maelezo yote
 
Back
Top Bottom