Msaada tutani: Bafu langu!

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
17,280
16,556
Hey~lo!

Sorry nimekuwa kimya naumwaaa shetani ashindww hataki me nisonge mbele na entertainment! Shindwa shetani wa magonjwa shindwaa!

Skumoja nipo na baby~sit watoto wq dadangu, hehe

Walipoenda kulala, shemeji alikuwa amesafiri, dada akachelewa kurudi from work ikabidi nilale pale

Kulipokucha nikaenda kuomba sabuni niog, nikaambiwa njoo uogee huku kwangu, mjeda nikadondoka master bathroom!

Kuingia mwe mwe mwe! Yani huko kuna shower gell mpaka ya miguuu

1. Shower gel ya kuanza kuoga baada ya kujimwagia maji

2. Cream shower gel ukishamaliza kutumia shower gel 1, inanukia hiyooo

3. Scrub shower gel kama unaona mwili wako unamikunjo kunjo hauna network umepoteza mawasiliano una scrubia sasa iyo ili ukae sawa

4. Foot shower gell kwa ajili ya kusugua miguuu tuuu

5. Bado sabuni za usoooo, facial scrubs, liquid soap, mweee
Utadhani nipo 6star bathroom

6. Zile ndude zile za kujisugulia zile kamba za kusugua mwili zile nzuri nzuri sijui sponge ya kuogea mwe kila rangi zimepangwaaa

7. Tisa kumi kuna meza nje ya shower place imejazqa Perfumes za kila aina, deodorants za kila aina gademit jaman nilijua haya mambo uraya uraya kumbe na bongo vepee!

Me nikijiangalia bafu langu kuna dodoki, na jiwe la kariakoo pale sokoni lile jeusi la kujisugua mgongoni, kuna sabuni ya mche mbuni kama sio alovera za kariakoo, nimemalizaaa... mmh umaskini jaman sheedah!

Nikatoka pale staki kutokaaa maji ya motoooo, natamani nilale bafuni kunanukia kama umande wa Mbinguni, mwe bafu bafu kweli hata ukisema unapigwa miti pale unafungua uchi woteee kama unazaaa gademit

Embu nambieni wana JF nyie mabafu yenu yapoje, au ndo mende na panya wanawachungulia kwa chini?! Au bafu ndo choo kama uswahilini kwetu?! Uuuwiii

Mabafu yenu classic au mende bafu?!
 
Sasa ukinyeshewa si ndo vizuri unaahirisha kuoga unasimama unatega tu hadi utakate then maji yako kwenye ndoo unarudi nayo ndani bajeti ya keshooooo hakuna kuchota maji,,,,raha tupu
Mi bafu langu lipo nje, mvua ikinyesha nanyeshewa, mlamho wake ni kuning'iniza gunia au taulo au kanga, wakati unaoga wanaopita njiani wanakuona unavyojimwagia na kopo. Karibu kwetu Money penny
 
Karibu geto kwangu tule panya hadi paka waone wivu
1_dirty_toilet_by_woodmillmiles+%282%29.jpg
.
 
Bafu langu la passport size...limejaa vicherema vya sabuni za kufulia..jiwe moja la mtoni..kakopo ka blue band na brashi ambalo ni kipande cha chandarua..
[HASHTAG]#KaribuKwetu[/HASHTAG]
 
Mi bafu langu lipo nje, mvua ikinyesha nanyeshewa, mlamho wake ni kuning'iniza gunia au taulo au kanga, wakati unaoga wanaopita njiani wanakuona unavyojimwagia na kopo. Karibu kwetu Money penny
Ahahahahaha
Nimecheeeka, jaman nyie mna vituko kweli
Asante ntakujaaa

Karibu geto kwangu tule panya hadi paka waone wivuView attachment 494389.
Yesu wangu nini hiki mpaka mwili umesisimka uuuwi

Sisi wa uswazi tumesha zoea mabafu yetu ya passport size maisha yanasonga.
09c525de033d8c33e202fc8eaa5dbd21.jpg
Ahahahahahha noma sanaaa

Hilo bafu ungeweka hata picha moja,,au umeliona kwenye movie.?
Mweee simu ilikuwa kwenyw chaja nikashindwa kupiga pichaaa
 
Bafu langu ukiingia lazima uimbe imbe bila hivyo ghafla bin voo mtu anaingia direct
Ahahahaha nakuelewa sana yale ya uswahili kwetu sio?! Ahahahaha

Bafu langu la passport size...limejaa vicherema vya sabuni za kufulia..jiwe moja la mtoni..kakopo ka blue band na brashi ambalo ni kipande cha chandarua..
[HASHTAG]#KaribuKwetu[/HASHTAG]
Ahahahaha mwe najuta kuandika hii thread nachekaje mwenyewe sasa kiru!

Nimependa kipengele ulichowaza kupigwa miti hapo bafuni.
Ur such a pervert! U so extra yow! Ahahaha
 
Mie bafu langu limejengwa kwa kwa miti ,na majani ya migomba mixer na mabua ya mahindi, kwa ndani limepangwa mawe , alafu kwa nje limezungukwa na nderema ( mboga za kutambaa). Mlango wake ni magunia ya sementi. Kuna zile nyuzi za kulowea samaki (mtego) ndio dodoki kwa akili ya kujisugulia.
Yaaan we acha tu
 
Mie bafu langu limejengwa kwa kwa miti ,na majani ya migomba mixer na mabua ya mahindi, kwa ndani limepangwa mawe , alafu kwa nje limezungukwa na nderema ( mboga za kutambaa). Mlango wake ni magunia ya sementi. Kuna zile nyuzi za kulowea samaki (mtego) ndio dodoki kwa akili ya kujisugulia.
Yaaan we acha tu
Uuuwi ahahahaha nimecheka
Mbona bafu langu kumbe zuri maana sio kwa hizi advertise, nilikuwa najua bafu langu kimeooo
 
Maelezo yako yamenifurahisha ila nimekereka hapo kwenye MWE MWE MWEE...!!Huwa nakereka mtu akiandika ivo
 
Back
Top Bottom