Msaada: Tumetapeliwa!

Kuna msemo wa kiswahili unasema "Ukitaka kutafuta nyoka anza kumulika miguuni pako". Mkuu hebu pia mfinye wife kidogo maana kwahiyo attachment uliyoweka hapo naona Kama wife mjanja mjanja kiaina.
neti=internet; mpunga=fedha/pesa. Una pointi ndugu
 
Aseah pole sana kila siku wezi wanabuni njia mpya ya kufanya wizi hawa mawakala wanaotembea mitaani wengi wanawalalamikia kwavitendo vya wizi wa mitandaoni

Kuna siku mtaan napoishi walipita hawa mawakala wakinadi wanasajili laini kwa alama za vidole sasa mke wangu aliwaita wamsajilie mmoja ya wale mawakala akawa naendelea na zoezi la kumsajilia mke wangu lakin mke wangu katika simu yake kaset typing prediction on alichokua anafanya yule wakala aliingia kwenye menu ya halopesa akawa anafanya muamala mara ikaingia sms kwenye simu sasa yule wakala akawa anataka kuifuta wife analazimisha lazima aisome dah ukawa mzozo kuna jirani akanipigia simu kwakua sikua mbali nikaenda faster kufika nakuta watu washajaa wakala kagoma simu isisomwe sms nikamwambia kama kweli hakuna tatizo kwann simu aikatazie mana hata kumpa mwenye simu hataki mpaka amalize usajili ikabidi nguvu itumike kuitoa lock jamaa kaamisha 765000 tulipompa kibano akaeleza njia mojawapo ni typing prediction yaan kama simu ikiwa na typing prediction on basi hawa vijana wanaibia watu kirahisi sana tuweni makini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu huo wizi ulitokea pia hapa Njombe jamaa yangu mke wake alikutwa na issue kama hii. Jamaa walikuja na issue za namba za tigo ila waliiba hela kupitia simbanking milioni 2 iliyokuwepo bank, pia simu ya mke wa jamaa yangu hao wezi waliishika kama anavyoeleza mhusika, ila baada ya wale wezi kuondoka simu iliblock sms, calls, simbanking ndo mke kushtuka yaani simu haziingii siku nzima. Kumbe wahuni walishafanya yao. Kwenda polisi kitengo cha cyber zile pesa zilikutwa zimetolewa na kutumwa kwa namba nyinginevya tajiri maarufu Njombe. Hakuna kilichofanyika. Muhimu usikubali kumpa simu mtu usiyemjua barabarani eti bundle la chuo na siyo mwanachuo!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
neti=internet; mpunga=fedha/pesa. Una pointi ndugu
Just connecting dots. Wife dezaini mtundu mtundu jamaa aende extra miles. Hata Kama hakuusika ila inaweza kumsaidia time nyingine.
 
Reactions: BRB
Kuna mawili hapo
1. Mke kashirikiana na huyo tapeli, wanawake sio wa kuwaamini, kiufupi hakuna mtu unapaswa kumwamini kiasi kile.
2. Jamaa aliyetapeli ni mzuri kwenye IT na aefanya kazi kwenye hayo mabenki.


Sasa ili kutaka kujua kama huyo mke hajashiriki fanya kama unamwambia utaenda kwa Mganga wa Kienyeji Kigoma au Sumbawanga na ukazie hapo hapo uone anaitikiaje ..!? Ukiona anakuja na wazo la kuicrush hiyo ishu jua tayari mwizi unaye ndani kwako


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…