Msaada: Transcript na Maombi ya Kazi

Msaada: Transcript na Maombi ya Kazi

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Wakuu Tume ya ajira wametoa tangazo la kazi, lakini kinachonishangaza katika maelezo ya jumla wamesema TRANSCRIPT hazitakubaliwa. Tume ya ajira wamekuwa wakichukua na kukubali maombi kwa transcript walichokuwa wanakikataa ni ile parcial transcript. Je wakuu hii imekaaje? wenye ufahamu na hili tafadhali wakuu.
 
Soma vizuri maelezo ya tangazo hilo utapata jibu. Usikurupuke pasipo kusoma between the lines.
 
Soma vizuri maelezo ya tangazo hilo utapata jibu. Usikurupuke pasipo kusoma between the lines.

"Transcripts", "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
Watakuwa wanamaanisha, mimi nilishawahi kutolewa kwenye chumba cha interview kwa madai kwamba sasa hivi utumishi haajiri mtu kama hana cheti.
 
Watakuwa wanamaanisha, mimi nilishawahi kutolewa kwenye chumba cha interview kwa madai kwamba sasa hivi utumishi haajiri mtu kama hana cheti.

walikuita kufanya nini sasa? hawa nao ovyo tu.
 
Ila kuna rafiki yangu alishawahi pata ajira kupitia hao hao utumishi, hakua na cheti wala transcript. alikua na provisional results tu. kama ipo ipo tu, msichoke wazee kuapply.
 
Watu wa ajira wana nongwa sana.Unakuta wanasema hawataki Transcript huku wengine wanaowajua wana waajiri kwa kutumia transcript hizo hizo.
 
Back
Top Bottom