Msaada: Toyota oppa imeanza matatizo baada ya kuifanyia service

Cipher op

Member
Jan 25, 2015
76
99
Msaada wenu wakuu gari yangu wiki iliyopita nimepeleka garage kuifanyia service. Service nilizofanya ni pamoja na kumwaga na kubadili oil na kubadili hydraulic na nyingine ndogondogo kazi ilifanyika vizuri kabisa. Tatizo limekuja baada ya kama Siku mbili kupita na tatizo lenyewe ni kama ifuatavyo
1.Nikiwasha gari inawaka lakini inatoa muungurumo kama machine ya dizel
2.Gari inawaka lakini nikiweka gia inazima
3.Nikitaka isizime basi ni lazima nikanyage kwenye kuongeza mwendo na haiwezi kumove
4.Nikiweka silence inazima yenyewe
NB: Gari ni Toyota oppa Auto na kabla ya service hiyo gari ilikuwa safi kabisa.
Msaada wenu wadau tatizo ni nini hasa na solution yake.
 
Sio mtaalamu sana ila ungesaidia basi kuongezea nyama hapo kwa kujibu haya maswali:

1.Toka ulimiliki umewahi fanya service kama izo mara ngapi na kwa fundi huyo huyo au?

2. Fundi "anaekufanyiaga" service umemuambia amesemaje?

Mengine watakuja wataalamu.
 
Angalia plug zako kama zina choma!!! Cheki pump kama ina fanya kazi inavyotakiwa!!! Mwisho uwe unafanya service kwa wakati bosi!!! Na kwa fundi anaye eleweka!!!
 
Angalia plug zako kama zina choma!!! Cheki pump kama ina fanya kazi inavyotakiwa!!! Mwisho uwe unafanya service kwa wakati bosi!!! Na kwa fundi anaye eleweka!!!

Mimi namefanya once in a year (km 10,000 ila sio Tz), oil na filters zote ziko poa. Ishu nadhani sio timing ya muda bali kilometa na aina ya lubricants
 
Sio mtaalamu sana ila ungesaidia basi kuongezea nyama hapo kwa kujibu haya maswali:

1.Toka ulimiliki umewahi fanya service kama izo mara ngapi na kwa fundi huyo huyo au?

2. Fundi "anaekufanyiaga" service umemuambia amesemaje?

Mengine watakuja wataalamu.
Tumia oil ya Bp,hiyo gari engine haitaki Petrol chafu. Safisha tank la mafuta kwanza
 
Back
Top Bottom