software ni maelekezo yanayofanya kifaa chako kifanye kazi na version ni toleo la hayo maelekezo. huwezi kubadilisha mtunzi alieandika hayo maelekezo (developer) ndio mwenye uwezo wa kuyabadilisha. ukitaka kubadilisha unatakiwa uende sehemu ulipoyapata hayo maelekezo utapata toleo jipya. sehemu hio inaweza kuwa store au website ya hayo maelekezo.
mfano mzuri software ni kitabu na version ni toleo la kitabu, kitabu kimoja kinakuwa na matoleo tofauti tofauti na software pia huwa na matoleo tofauti tofauti. ili upate toleo jipya la kitabu itabidi uende dukani ukanunue kitabu kipya (hutaandika mwenyewe) hivyo hivyo upande wa software ili uibadilishe upate software mpya itabidi udownload/ufanye update toka store kama playstore au website mbali mbali ambazo wamehifadhi hio software