Pole sana ndugu yangu kwa tatizo. nimeshangaa sana comment za watu, mafundi wengi wanakimbilia kupiga window wakati kupiga window inaharibu sana harddisk, yaan kupiga window ni solution ya mwisho kabisa mtu anatakiwa ku consider, kama ni hospital basi tuseme mgonjwa ndo inabidi aingie ICU. mimi nataka kuwaambia watu, je ukuta wa nyumba yako ikimeguka kidogo tu utabomoa ukuta wote ujenge upya au utaweka kiraka na kusawazisha sehemu hiyo? hapa bongo mafundi wengi wanajua window ndo solution, lakini nakusifu kwa kuwa na moyo huo wa subira. mimi nitakupa solution. kwa troubleshooting ya haraka haraka, madhali ina detect kwa computa zingine na kwako ndo haikubali ku connect, hapo moja kwa moja tunasema modem ni nzima, na tatizo ni computa yako. sasa tatizo lipo wapi hasa? tatizo ni kwenye drivers ya hiyo modem yako kwenye computa yako, aidha itakua imeliwa na kirusi au ime corrupt. chakufanya ni kutoa drivers na ku install tena, usi uninsatall kawaida maana hua inabaki mara nyingine kwenye system. nenda MY COMPUTER, right click ingia manage, utaona device manager, hapo ndo kuna drivers, angalia hiyo modem ipo kwenye port gani, dan nenda na uitoe manually, ukimaliza restart laptop yako halafu install upya. ikikataa hiyo naomba ujibu nikupe solution ingine, actually solution zipo nyingi, mgonjwa akiumwa tumbo inaweza kua ni typhoid, au minyoo, au amekula kitu kibaya, au kavimbiwa au hata njaa pia, kwahiyo vyote vinawezekana. lakini kupona lazima, kwa sasa usipige window ingine boss.