Msaada: Taratibu za kupokea mzigo kutoka UK kupitia Kenya ni zipi?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Siyo utani ni shida ya kweli...

Kuna mtu kanifuata hapa anasema katumiwa parcel kutoka UK na imefikia Kenya

Watu wa Kenya wamemtumia sms Whatsapp wamemwambia aende akachukue mzigo wake ndani ya saa 12 akiwa na orijino copy ya ID.

Kinachomtatiza ni process za kufika hapo Uwanja wa Jomo Kenyatta anahisi muda hautoshi amejaribu kuwa-sms wampe maelekezo zaidi lakini meseji haioneshi kusomwa (hawapo online)
 
Siyo utani ni shida ya kweli...
Kuna mtu kanifuata hapa anasema katumiwa parcel kutoka UK na imefikia Kenya sasa watu wa Kenya wamemtumia sms Whatsapp wamemwambia aende akachukue mzigo wake ndani ya saa 12 akiwa na orijino copy ya ID. Kinachomtatiza ni process za kufika hapo Uwanja wa Jomo Kenyatta anahisi muda hautoshi amejaribu kuwa-sms wampe maelekezo zaidi lakini meseji haioneshi kusomwa (hawapo online)

Utapeli huo,
 
Siyo utani ni shida ya kweli...

Kuna mtu kanifuata hapa anasema katumiwa parcel kutoka UK na imefikia Kenya

Watu wa Kenya wamemtumia sms Whatsapp wamemwambia aende akachukue mzigo wake ndani ya saa 12 akiwa na orijino copy ya ID.

Kinachomtatiza ni process za kufika hapo Uwanja wa Jomo Kenyatta anahisi muda hautoshi amejaribu kuwa-sms wampe maelekezo zaidi lakini meseji haioneshi kusomwa (hawapo online)
yakipita hayo masaa 12.. itakuwaje ?
 
Utapeli huo,
Hebu nifafanulie zaidi maana hata mimi nilimwambia kuwa hawa ni matapeli akaniaminisha sana kuwa siyo utapeli... Kuna mpaka risiti yenye jina lake, aina ya vitu vilivyomo kwenye parcel, sehemu ulipokusudiwa kwenda, gharama za kutuma, na mambo mengine kibao! Nilichomjibu ni kwamba Mimi sina uzoefu na maswala haya yanayohusu ndege au maswala ya kimataifa
 
Siyo utani ni shida ya kweli...

Kuna mtu kanifuata hapa anasema katumiwa parcel kutoka UK na imefikia Kenya

Watu wa Kenya wamemtumia sms Whatsapp wamemwambia aende akachukue mzigo wake ndani ya saa 12 akiwa na orijino copy ya ID.

Kinachomtatiza ni process za kufika hapo Uwanja wa Jomo Kenyatta anahisi muda hautoshi amejaribu kuwa-sms wampe maelekezo zaidi lakini meseji haioneshi kusomwa (hawapo online)
Ebooh huu ujinga mtaachaga lini?
Bila ya shaka huyo aliyetuma mzigo mmejuana naye FB !!
We subiri hao wakenya wakutumie text kwamba uwatumie 50K Hadi 200K kupitia safaricom mpesa ili wauship mzigo kuja Tz afu wewe ukapokelee pale JNIA.
Ukishatuma tu ndio wanakublock mazima kule Whatsapp na muhusika naye anakublok
 
Hebu nifafanulie zaidi maana hata mimi nilimwambia kuwa hawa ni matapeli akaniaminisha sana kuwa siyo utapeli... Kuna mpaka risiti yenye jina lake, aina ya vitu vilivyomo kwenye parcel, sehemu ulipokusudiwa kwenda, gharama za kutuma, na mambo mengine kibao! Nilichomjibu ni kwamba Mimi sina uzoefu na maswala haya yanayohusu ndege au maswala ya kimataifa
Ndg. Kama ni wale jamaa wa kukutana whatsap, hata mimi nilikutana nao. Dada mzuri kutoka Australia kumbe ni picha tu ila ni wahuni wa Nigeria na Senegal nililijua hilo baada ya kugoogle namba kiunganishi ya dada yule aliyesema ni kutoka Australia kumbe ni code number ya Senegal. Na kabahasha kangu kangetoka Australia na ningekapokelea Senegal. Nilipogundua ni matapeli wa mtandaoni nikaachana nao.
 
Inashangaza sana huyo mtu ni ww mwenyewe afu kwa ujinga wako utatapeliwa kizembe sana
Umewahi kuniona Facebook mdau? Umewahi kuniona mtandao wowote wa kijamii kinyume na huu? Unanijua kwanza, au unabwabwaja tu?
 
Ebooh huu ujinga mtaachaga lini?
Bila ya shaka huyo aliyetuma mzigo mmejuana naye FB !!
We subiri hao wakenya wakutumie text kwamba uwatumie 50K Hadi 200K kupitia safaricom mpesa ili wauship mzigo kuja Tz afu wewe ukapokelee pale JNIA.
Ukishatuma tu ndio wanakublock mazima kule Whatsapp na muhusika naye anakublok
Unafaa kuwa mwalimu kwenye maswala haya lakini punguza ukali wa maneno basi
 
Ndg. Kama ni wale jamaa wa kukutana whatsap, hata mimi nilikutana nao. Dada mzuri kutoka Australia kumbe ni picha tu ila ni wahuni wa Nigeria na Senegal nililijua hilo baada ya kugoogle namba kiunganishi ya dada yule aliyesema ni kutoka Australia kumbe ni code number ya Senegal. Na kabahasha kangu kangetoka Australia na ningekapokelea Senegal. Nilipogundua ni matapeli wa mtandaoni nikaachana nao.
Mimi nilikutana na jamaa hivyo hivyo anajidai yeye ni boss wa UK nikamuuliza mbona code namba ya Nigeria akajing'atang'ata hapo nikamwambia sihitaji kuwasiliana naye mpaka aniambie amepata wapi namba yangu na ana shida gani... Akasepa mazima baadae nikajaga kugundua kumbe ni zile vpn za internet za bure nikitumia ndio napokea wageni wengi sana Whatsapp basi nikaziondoa kwenye simu yangu haraka sana

Huyu raia aliyeniletea hii hoja yake inaonekana wamempania (wameanza kumpangilia) tangu muda sana maana nimempa mifano mingi ya utapeli lakini ananiamini nusunusu bado anatamani kuendelea nao anasema yeye ameanza nae muda sana huyo binti kuwasiliana naye (na walianzia huko kwenye facebook)
 
Mwache ananyota ya kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom