Msaada tafadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tafadhari

Discussion in 'JF Doctor' started by katutumla, Jul 16, 2010.

 1. k

  katutumla Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Ni post yangu ya kwanza na naanza na tatizo!
  Nina ndugu yangu ninayemsaidia (dependant) amepata ugonjwa wa kutokwa usaha (well ni maji mazito ya rangi ya njano, yananata kiasi) kwenye masikio. Mwanzo alikuwa anasikia maumivu makali kwenye sikio la kulia na baadaye likaanza la kushoto. Tumekwenda hospitali akapewa Amoxyclav, Brufen na Rantec ambazo ametumia kwa siku tano. Sikio la kulia limeacha kudischarge lakini la kushoto bado. Anasema halina maumivu lakini linatoa majimaji hayo ambayo yana harufu mbaya. Hii ni wiki ya pili sasa.
   
 2. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ngoja tuwaachie wataalamu uncle. Ila ningependa kukupa pole kwa kuuguza.

  MUNGU akutieni nguvu.
   
 3. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  UMRI wa mgonjwa,...
  Mbali na maumivu alikuwa na dalili gani nyingine?exp mafua ,kujisikia kama masikio yameziba,,,
  kabla ya hapo alikuwa ana tabia ya kujichokonoa masikio kwa vijiti?
  Au alikuwa ana tabia ya kuogelea ?
  Hata hivyo kutoka usaa kwenye masikio kwa walio wengi husababishwa na maradhi yajulikaanayo kama Otitis media na kwa wengine otitis external,.

  kwa habari zaidi unaweza kulink hapa zipo too general lakini sio mbaya
  Otitis media - Wikipedia, the free encyclopedia

  Kuhusu matibabu,mara nyingi huzingatia chanzo sababishi cha hayo maradhi,kama ilikuwa ni bacteria,hutolewa dawa nyepesi ya mwanzoni,huku yakisubiriwa majibu ya culture,ya huo usaa.,..
  kama ni virus basi ni vile vile kuondoa ugonjwa sababishi kwanza.
  Hyo matibabu ni mazuri,...lakini sehemu na sehemu hutofautiana kimatibabu.,..
  kipindi kile nafanya kazi nyumbani na hata huku nilipo sasa suala la kutoka usaa hutibiwa kwa kutumia ALOGARITHM IFUATAYO Three AAA and one B , ..Antibiotic,Antihistamine[za kuzuia mzingo au allergy] and Anticongenstant[hizi huwa ni nosal drops].,....na pia Boric acid ni muhimu katika kurekebisha Ph ya sikio,.hivyo drops zake hudondoshewa kwnye sikio mara tatu kwa siku.
  Rantec ??Huyu mgonjwa ni mwanaume au mwanamke?na umri wake.,..??
  Mwisho nakushauri akienda kuoga azibe masikio yote kwa pamba asiruhusu maji yaingie kwenye sikio...
  SIJUI uko mkoa gani.,Lakini ni MUhimu kuwaona madaktari wanaoitwa ENT doctors,Hao wapo BUGANDO,MUHIMBILI,KCMC na MBEYA,...mikoa mingine hawapo hiyo ni elimu iliyojificha na madaktari wake ni wachache.
  HATA HIVYO KUNA UMUHIMU WA KULIANGALIA HILO SIKIO kwa ndani labda sababu inaweza onekana
  kuna kitu kinaitwa Cholesteatoma hicho pia ni kisababishi kimjawapo,..
  Hata hivyo mpeleke kwa wataalamu wamuangalie,...huo usaa ukuendelea kutoka kwa muda mrefu anaweza kupata mastoiditis,...hapo amekwisha,...mtacheza na ngoma ya kutoka usaa mpaka uzeeni,...Muwahishe ,...
   
Loading...