Msaada tafadhalini wa dawa nzuri ya tatizo la magoti ya Wazee kukosa mchuzi au ute wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Natanguliza Shukurani zangu kwa wote mtakaonisaidia kwa majibu yenu ya Kimatibabu ili nami niweze kumuokoa kama siyo hata kumsaidia Mgonjwa wangu.

Nina Bibi yangu anasumbuliwa mno na tatizo la Magoti yake kukosa ule mchuzi / ute wake hivyo inasemekana magoti yake yanasuguana kwani hiyo ' Grisi ' au huo ute / mchuzi haupo na kiukweli yanamsumbua sana hadi anakosa raha na kibaya zaidi Mgonjwa wangu mwenyewe anapenda mno Kutembea.

Nitashukuru kama nitapata ushauri wa dawa za Hospitalini za Yeye kununua na ambazo pia hazina gharama sana kutokana na hali Yetu ya Kiuchumi sasa kwa Watanzania au nikipata pia zile dawa za Kienyeji au zile za mchanganyiko wa matunda au mboga fulani nitawashukuruni pia.

Karibuni na nayasubiri majibu yenu ya Kitabibu na Kiutaalam kabisa ili nami nimtibu Bibi wa GENTAMYCINE. Umri wake sasa ni miaka 70 na uzito wake ni kama Kilo 92 hadi 99 hapo.

Mbarikiwe nyote!
 
Supu ya Kongoro na bamia vipi mkuu

Kajaribu hizo lakini bado na ndiyo maana nimeomba kama kuna dawa zingine labda za asili / za kienyeji ambazo anaweza kutumia kumasaidia au hata zile za Kidaktari. Hata hivyo nakushukuru na akhsante sana Mkuu kwa ushirikiano wako wa kunijibu. Ubarikiwe!
 
Back
Top Bottom