Msaada tafadhali

Msaada tafadhali

johye

New Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
2
Reaction score
0
Bila shaka mtakuwa mpo wazima kuna tatizo linanitatza sana nimeleta kwenu mnipe mawazo cha kufanya.

Nina girlfriend wangu tupo muda mrefu sana na nina malengo, baada ya kumaliza chuo alikuwa bado hajapata kazi, mambo yake yote nilikua namtimizia, kwa bahati mbaya simu yake ilialibika ghafla akawa hana simu ilibidi nimpe simu moja ya kawaida ya nokia mimi nikabakiwa na smart phone, akaomba nimununulie simu, nikamwambia nitakununulia nipe muda sasa mambo yameingiliana, ikapita kama miezi miwil hivi, akanikumbusha nikamwambie nivumilie.

Akafanikiwa kupata kazi katika kampuni fulani, akafanya kazi kama mwezi, akanunua simu bila kuniambia, akaomba tukutane sehemu, nikafanya hivyo baada ya maongezi, akanionyesha simu aliyonunua nikashangaa sana kwa nilimuliza simu kama hiyo nilitaka kukununulia ulisema hiyo simu huwezi kutumia, akasema sinajinsi nitatumia kwa muda.

Tatizo likaanza, nikamuuliza kwanini hukunipa taarifa akasema nimetumia hela yangu, kwanza nimekuomba muda mrefu ununulie umeshindwa nikupe taarifa ya nini maneno yote hayo alinipigia simu wakati yupo kazini kwake kwangu mimi niliona kama dharau kwangu kama aliona hilo kwanini asinitafute manually, baada hapo tuligombana kwenye simu tukiwa tunaongea, mpaka sasa tuna week hatujaongea.

Nahitaji mawazo yenu.
 
wewe umeahidi umeshindwa kutimiza unajua amepata kazi kumbe ndo ilomfanya anunue simu sasa we kinakuuma nini km kaamua kukupunguzia majukumu? we umesema mlionana akakuonesha simu mara amekupigia simu sjui hakufanya nini nini manually sasa ndo nini
 
wewe kijana mwanamke akishaanza majibu ya kibwegee kaa ukijua kuna mjanja anamgegeda. kula nduki
 
Sisi wanawake tuna kasumba moja mpaka tuseme sikutaki ni mtihani

kigezo cha mwisho kwamba hutakiwi ni jibu kama hilo

umeuliza umenunua hujaniambia kakwambia hela ujanipa

kesho utamkuta na gari atakwambia hela ujampa

kwa KIFUPI KUCHAPIWA SIRI YA NDANI...UR NO LONGER NEEDED
 
kaeni muongee muyamalize kama lengo lake si kuachana atakuelewa ila kama wameshawahi wajanja ndo basi tena
 
Mtakuwa mnacheza kombolela tu ninyi...

Utoto raha sana..
 
Kama simu umeshindwa kumnunulia unalalamika nini?
 
Sisi wanawake tuna kasumba moja mpaka tuseme sikutaki ni mtihani

kigezo cha mwisho kwamba hutakiwi ni jibu kama hilo

umeuliza umenunua hujaniambia kakwambia hela ujanipa

kesho utamkuta na gari atakwambia hela ujampa

kwa KIFUPI KUCHAPIWA SIRI YA NDANI...UR NO LONGER NEEDED

wewe kijana mwanamke akishaanza majibu ya kibwegee kaa ukijua kuna mjanja anamgegeda. kula nduki[/QUOTE
Unaonaje ukiyafanyia kazi haya?
 
Mdau pole kwa mkasa, kaeni muongee muyamalize ila uyo dada atakuwa ana lake jambo kama kanunua simu y asikwambie kwa ninavyojua atakuwa kuna mchezo mchafu anakuchezea chekecha mawazo kiutu uzima
 
yaani wataka hata mshahara wake akueleze anafanyia nini kweli?
Angekuwa hana kazi sawa ungeuliza hela kapata wapi, ila mtu ana kazi yake kabisa.
Huo ni utoto na msipokuwa makini huo ndio mwisho wenu hapo, maana magomvi hayataisha.
 
Pole....ila hapo sidhan kama kuna mapenzi ya dhati...kwahiyo ungemnunulia smu angeendelea kukudanganyadanganya badae ungeshindwa kingine angeanza nyodo
 
Dada hajielewi huyo chapa lapa. Hata kama amejinunulia angekueleza at her own time na decently. Simu tu anamissbehave je ingekuwa kajinunulia gari?
 
Hapoh kama una malengo nae duh jaribu kusahau taratibu maana hilo jibu lake la mwisho ni kielezo tosha yeye hana shida na wew alikuwa anatafuta tu mahali pa kutokea si ajabu hata hapo kazini kwake ndio kuna mjanja kakupokonya na tonge lako usisubirie kuambiwa sikutaki chukua hatu kabla hajakuumiza zaidi
 
Back
Top Bottom