noella,
Paloma et al...
Sijui nisemeje, hali ya rushwa (kuomba/kulazimisha/kutengeneza mazingira ya) Tanzania sio jambo geni. Kila mtu aliyepewa wadhifa fulani anataka kutumia nafasi ile kujinufaisha - hata kwa lazima ikibidi.
Hali hii ipo wizara ya ardhi, bandari, TRA, hospitalini na karibu kila sekta hapa nchini. Si juzi tu
lara 1 ametumabia ishu kama hii ya rushwa?
Polisi kwa upande wao wamekuwa wahanga wakubwa wa malalamiko haya hasa kwa kuwa wao wana-direct interaction na raia wengi kwa nyakati tofauti na katika matukio tofauti.
Na wao kama watumishi wengine wa nchi hii wameona na wao wachukue chao mapema kwa nafasi walizopewa. Ubaya wake sasa ni kutofanya upelelezi wowote bila kutolewa, kutochunguza tukio lolote lililoripotiwa bila kuona maslahi - ya kifedha- kwao, yani hawafanyi chochote ambacho there's nothing in it for them.
najua hapa si mahali pa kuanza kuelezea kwanini wanafanya hivyo na wala si wakati muafaka wa kuanza kuelezea nini kifanyike kuepusha jambo hili.
Ninachoweza kuwaeleza kama raia wema ni hiki, "Kuijua haki yao, kuijua sheria ni silaha kubwa kwako dhidi ya unyanyasaji wowote." Rushwa tuliiotesha wenyewe, tuliipalilia wenyewe na tunaikuza wenyewe. Hivyo basi hata kuitokomeza ni jukumu letu wenyewe.
Tusiwe warahisi kutafuta solution za mkato hasa pale tunapojikuta mikononi mwa polisi. Tambua haki zako. Kama kweli uko kwenye kosa basi isiwe ndo wakati wa kumtoa buku ili usepe fasta! nenda kalipe fine kituoni.
Dada
noella, situation yako ni ngumu mtu kuweza kukushauri kwani hujaieleza kinagaubaga. Bado ninabaki na maswali mengi kichwani.
- uhusiano wako na huyo akutishiaye maisha?
- alikutishia kwa maneno, simu, sms au?
- kwa nini umeamua kufunga kesi?
-nk nk...