Msaada tafadhali naomba niwe mkweli

Msaada tafadhali naomba niwe mkweli

JONASON

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
461
Reaction score
706
Ndugu zangu wanajamii forum naomba anayejua au mwenye access na mtu au kiumbe chochote mwenye kutoa utajiri ambaye ana mashart yoyote yasiyo husisha kuuwa au kutesa mtu mwingine au ndugu yako aniunganishe au tuwasiliane pm au hatakujiunga freemason bas anisaidie huko maana nimechoka na unasikini, dhiki na kudharauliwa..​

Mimi ni kijana nimesoma mpaka level ya shahada ya kwanza nimemaliza sasa Nina miaka mitano toka nimemaliza nimeandika barua za maombi nyingi toka nimemaliza takriban kila siku nafanya maombi sio chini ya taasisi kumi mpaka saba nimeshaomba kujitolea ila ni chenga tupu nimejaribu kutafuta hata contact za matajir wakubwa nikaomba wanipe shavu hata kuuza duka ila hamna wote kimya na Mimi siangalii kiwango cha mshahara ili mradi niya mudu maisha nitoke nyumbani kwa wazee niweze hata kujitegemea maana chuoni nilikosa mkopo Wa serikali ikabidi wazee wauze vitu kadhaa niweze kusoma nije niwasaidie ila bado nimekua mzigo na mtaji hawana Wa kunipa na bado kuna madogo wanataka ada nimejitahidi kuchukua kila hatua nimezunguka interview nyingi nimejikuta namaliza nauli tu na Mimi ni mtu Wa dini nimefika hadi Tanganyika Pecker's kawe kwa Boniphace mwamposa nimewekewa mikono nikaombewa ila bado sana sana sasa kaka , Dada , wadogo na wazazi wanaona Mimi ni mtu Wa ajabu kwa vile sina muendelezo mzuri toka nimemaliza elimu yangu ya shahada japokua nasaidia suala la Kilimo na kupiga vibarua kupata fedha hata za kununulia mashati na suruali na moka za kuendea ktk usaili ila napoteza muelekeo napambana kwa njia ambazo sipati kitu na pia nilipitia JKT kwa mujibu Wa sheria hivyo nidhamu ipo nikiomba hata kazi za ulinzi sipati.​
Basi ombi langu lilikuwa ni hilo wana jf wenzangu mnisaidie sisi sote ni ndugu na Mungu ni wetu ..NB: ushauri na maoni naruhusu ila usiniseme vibaya wala usiniongelee vibaya unitoe katika mood ..Nawasilisha​
 
Mkuu kama wewe ni wa kwa Mwamposa basi tatizo lako limeshajulikana.
 
Usikate tamaa Kaka, mafanikio huja ukizingatia kujituma... Jaribu kupitia mada kadhaa humu ujifunze watu wanavyopitia misukosuko kabla ya kusimama imara



Pambana mpaka kieleweke
8588.jpeg
 
Unakata tamaa kirahisi man....wenzio wana miaka zaidi ya kumi mtaani na hawana presha...calm down boy
 
Ndugu zangu wanajamii forum naomba anayejua au mwenye access na mtu au kiumbe chochote mwenye kutoa utajiri ambaye ana mashart yoyote yasiyo husisha kuuwa au kutesa mtu mwingine au ndugu yako aniunganishe au tuwasiliane pm au hatakujiunga freemason bas anisaidie huko maana nimechoka na unasikini, dhiki na kudharauliwa.
kama kungekua na masharti mepesi kama ambayo unakusudia kumaanisha hapa bas kila mtu angekua tajiri
 
Acha ujinga wewe. Nenda Njombe ukalime parachichi zile ambazo zinazaa throughout the year. Panda miche mia tu. Thank me after 30 months
 
Mkuu wengi tunalia Tukaze tu mkuu ndio uanaume. Umejaribu hata umachinga mkuu?
Uko mkoa gani?
 
Umeshakata tamaa ya Maisha.

Hiyo haitakiwi, usikate tamaa.

Na usiwaze sana kuajiriwa, wakati unasikilizia mipango yako jaribu pia vishughuli vingine vya kubangaiza.

Kuwa mtu wa kujichanganya sehemu tofautu tofauti ili ukutane na watu tofauti tofauti.

Kuna wakati kujichanganya kwako, ndio na Mipango mingine ya kimaisha unaweza kukutana nayo.

Ondoa mshipa wa aibu, na wala usichague shughuli ya kufanya.

Kupambana kwako na Maisha ndio siri ya mafanikio yako.

Hayo mengine unayoyafikiria yatakuja kukutoa kimaisha inaweza ikawa sababu ya wewe kuja kutapeliwa kidogo chako na hao ambao unaofikiri watakuja kukuunganisha katika njia za kuupata Utajiri
 
Back
Top Bottom