Msaada tafadhali: Mimi ndio kaka na sijui niamue vipi

Msaada tafadhali: Mimi ndio kaka na sijui niamue vipi

beleza

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
397
Reaction score
144
Kuna mdogo wangu wa kike (baba moja mama mmoja) aliolewa lakini katika ndoa ile familia yetu yote ilikataa kuwa pamoja na yeye kwa sababu mume wenyewe alikuwa haeleweki kwa tabia zake za kuoa na kuacha kila mahali. Hilo tulilijua baada ya kumchunguza na tutamwambia huyu mdogo wetu juu ya tabia ya huyo mwanaume lakini akasema yeey anamtaka hata kama ana tabia gani.

Poa baba na mama na familia yote ikamsusia na akaenda kwa mzee moja ndio akamuomba aende kwa baba ili apewe idhini amuozeshe yule mzee akafanya kama alivyomuomba na wakafanya ndoa yao ya aina yao. Sasa baada ya miaka kupita na kufanikiwa kupata watoto watatu na yule mume na kujenga nyumba yao hatimae yule mume kamuwacha na kamwambia asifike pale penye nyumba yao.

Poa mimi nikamwambia njoo nyumbani utulie kwa kweli akafika nyumbani na akatulia, sasa ni kama miezi minne ivi imepita. Sasa cha ajabu juzi nimepigiwa simu wanasema karudi kule kwenye nyumba yao na baada ya kufika kule na aliyekuwa mume wake kupata taarifa akampigia mtu wake wa karibu na kumwambia aondoke na haraka sana yeye hamtaki ata kumsikia.

Mimi nikaona ni sawa sababu siameshaachika tayari) tatizo huyu mdogo wangu anataka kukaa na watoto wake lakini huyo bwana alimwambia ukichukua watoto usiniulize kitu au nikiwachukuwa na wewe usiniulize kitu. Sasa na huyu mdogo sijui nimsaidieje kwa kweli.

Tatizo nalionalo, kwanza ni mbishi sana, kisha hataki ushauri wa mtu.

USHAURI WENU TAFADHALI
 
Nyumba waliojenga wote kama mume na mke inamuhusu huyo Dada ako na sheria zipo bila kusahau hao watoto wazazi wote pande mbili wanahusika kuwahudumia haijalishi wanaishi kwa nani... Fateni sheria nahisi itawasaidia zaid kwenye swala la watoto na hiyo nyumba,kuhusu ubishi wake we usichoke kuongea nae mtumie na watu waliowazid umri kumshauri yanayofaa,....akiwa haelekie muache dunia imfunde kwa mara ya pili
 
kuna mdogo wangu ....tatizo nilionalo mm kwanza ni mbishi sana.kisha hataki ushauri wa mtu.USHAURI WENU TAFADHALI .
Mkuu ni mdogo wako au ni wewe umekuja kiaina!!anyway nadhani pia umeingia jukwaa ambalo sio sahihi...hope utapat ushauri...
 
Thanxs sabrina.hapa nimependa sana.(akiwa haelekei muache dunia imfunde kwa mara ya pili).tatizo cmu zake zote kazima kwa iyo nimejaribu kumtafuta mpaka kwa watu wake wa karibu nimeshindwa na mm nipo mbali sana na yy.

jengine haya mambo yametokea ZNZ sasa mm sielewi taratibu za kule kama ni sawa na huku bara juu ya hiyo sheria ya nyumba.sababu kama angelikuwepo huku ni rahisi kulitatua na kupata haki yake jee kwa hilo unaweza kujua kama na kule anaweza kupata haki yake kwa sheria za znz?
 
Kitei tei mm nq braza wake wa damu.yaani kwa kweli MAMA ndio yupo na mawazo juu ilo jambo na yeye anataka niende kulitatua ila cjui niazie wapi .kwa kweli linatuumiza vichwa familia yote.uahauri wenu ndio nahitaji kamanda
 
Kuwa na sista kazi sumtymz..nashukuru masista wangu wameolewa na wako happy na ndoa zao...mkuu usichoke kumshauri..coz mwisho wa siku akipata tatizo familia ndo inahusika..kuhusu watt na mali afwate sheria tu
 
Sawa Kaboom lkn ningependa kujua kuhusu watoto na mali sheria na kule visiwani (znz)na huku juu ya mali na watoto ni zile zile au ni tofauti?hapo ndio nashindwa kuenda sababu kama ni tofauti unafikili nitamsaidiaje ili apate haki yake?duuuh majanga plus kwa kweli
 
Mwambie aende ofisi za TAWLA apewe ushauri wa kisheria. Haiwezekani mtu afukuzwe kama "mbwa" kwake. Msaidie mdogo wako ktk kipindi hiki kigumu.
 
Ngwananzengo na TAWLA kule Zanzibar ipo?wanaojua msaada tafadhali sana
 
Back
Top Bottom