Msaada tafadhali kuhusu sheria za barabarani

molwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
425
Reaction score
456
Habari za jioni wanajukwaa! Nahitaji kujuzwa kuhusu sheria hii: Abiria anaekaa kiti cha nyuma baada ya siti za mbele ni lazima afunge mkanda?? Maana nimekutana na utata leo jioni, kuna trafiki alinisimamisha abiria wangu wa nyuma hakuwa amefunga mkanda, kwa jazba kachukua leseni na kadi kapeleka kwa bosi wake nikalipe faini, nikamweleza bosi kuwa abiria asiefunga mkanda yuko siti ya mbele, akasema sina kosa akanirudishia vitu vyangu nikaondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abiria yeyote anayepanda gari lako pamoja na wewe mwenyewe kama dereva, ni sharti muwe mmefunga mikanda wakati wote muwapo barabarani. Hii tabia ya kutofunga mikanda kabisa, ni jeuri tu iliyojengeka hapa kwetu na kama matrafiki wakifuata sheria kama zilivyo vilio vya kuonewa tutavisikia sana.
 
Abiria anaekaa viti vya nyuma HALAZIMIKI KISHERIA kufunga mkanda. Ila kiusalama abiria wote wanatakiwa kufunga mkanda.
 
Ile mikanda sio mapambo imewekwa kwa ajili ya usalama wa abiria na dereva makini hawezi ondoa gari bila kuhakikisha kila aliyempakia amefunga mkanda kwa usahihi
 
Nashukuru sana kwa maelezo yenu! Kuanzia leo wote nitakaowapakia lazima wafunge mikanda! La sivyo siondoi gari! Sitakagi usumbufu mie[emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya usalama wa barabarani ya Tz, sura ya 168 inamtaka abiria yyte aliyekaa siti ya mbele (pamoja na dereva) kufunga mkanda wa usalama.

Sheria hii ipo kimya kuhusu wale watakaokaa siti za nyuma. Hii ni kwenye magari madogo yanayoendeshwa chini ya daraja B na D la leseni
 
Nikiwa mtunga sheria nitapendekeza magari ya bushi yawe na mikanda mpaka kwenye butI maana dah
 
Abiria wote mnatakiwa kufunga mikanda.... wooote na dereva (kama mnajali usalama wenu lakini)
 
Acha kukurupuka
 
Hivi wakuu, sheria inasemaje juu ya mtoto kukaa siti ya mbele, ??
Mtoto wa miaka 2 and above
 
Hivi wakuu, sheria inasemaje juu ya mtoto kukaa siti ya mbele, ??
Mtoto wa miaka 2 and above
Haruhusiwi kukaa mbele
Pia haruhusiwi kupakiwa kwny bodaboda na akiwa chini ya miaka 12 hatakiwi kupakiwa kwenye bajaji bila kuwepo mtu mzima
 
Nauliza tu jamani seat ya nyuma alietengeza gari hakuweka mkanda? Ikiwa jibu ni ndio basi nafikiri nimeeleweka namaanisha nini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hofu kubwa kwa sit ya mbele ni uwezekano wa Dereva na abiria wake kujipiga kwenye kioo cha mbela (Wind Screen) na kutoka nje ya gari
Lakini kwa siti ya nyumba hata kama utarushwa utaishia kujigonga kwenye viti vya mbele

Hivi ushajiuliza kwa nini Airbags ziko viti vya mbele tu?

molwe
 
Na mie dereva wa mwendokasi pia unamaanisha nisitoe gari hadi wote wafunge mkanda? Na rafiki yangu anayeendesha mabasi ya Mbagala nae inamhusu? Huku kutegemea mapato ya barabarani sio sawa kabisa. Yaani trafiki wanawinda mjini utadhani kama wakoloni walivyokuwa wakiwinda tembo wetu. Trafiki 10 wanakaa sehemu moja wanavizia magari, what a high level of misuse of our resources is that??
 
Unadhani hakuna gari zenye Airbags siti zote?

Zipo gari chache sana zenye Airbags kwenye siti za mbele na nyuma, tena ni zile gari zenye kubeba viongozi na watu wenye pesa za maana (Expensive cars) swali ni kuwa Kama ni za muhimu sana kwa abiria wote, kwa nini ni gari chache tu ndio zina hizo Airbags,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…