Software ya benki unayoongelea inatwa Core Banking System hii ni software tu, hii ndo inatunza accounts za wateja pamoja na zile za GL za benki na ndo Debits na Credits zinafanyika katika hiyo software.
Pia software hii inaruhusu software zengine kufanya Debits/Credits kwenye account hizo kupitia njia tofauti kwa mfano File Uploads unaipa Core Banking System file inayoiambia idebit au Icredit account zipi, WebServices Core banking inaruhusu sofware nyingine kuconnect katika WebService na kuipa commands ambazo zinaeefect accounts.
Kwa njia hii unaweza ukawa na Core Banking System ya kampuni moja lakini ikafanya kazi na Software za kampuni nyingine kwa mfano ATM au Mobile Banking inaweza kuwa ya kampuni nyingine bila tatizo.
Core Banking System popular haziko nyingi duaniani kwa kuwa ni soko gumu sana kuingia na kupata wateja.
Mfano ni
FlexCube ya Oracle
Finacle ya InfoSys
SAP for Banking ya SAP
T24 ya Temenos
Kwa bahati mbaya hizi Software hautaweza kuzipata wala kuziinstall kwenye machine yako, na hata ukifanya kazi benki kwa hapa TZ hautaruhusiwa kuzigusa kiundani maana mikataba yake ni kwamba modification zote zinafanywa na kampuni yenyewe huko walipo (Mostly India) au wanamleta mtu wao.