Msaada: Sihitaji advance tena, nataka niende chuo(college)

Pure Scientific

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
716
643
Wakuu nmemaliza kidato cha nne mwaka Jana sasa kutokana na sababu zipo nje ya uwezo wangu sitaki kusikia chochote kuhusu advance hivyo nataka nikasome diploma ya clinical officer, pharmacy, au laboratory technical kwenye vyuo vya serikali ila msaada wangu kwenu sijui naanza wapi hadi kufika hatua ya kuingia chuo hata ada na vyote vya muhimu

-matokeo yangu ni kama yafuatavyo physics-c Chem-c bios-c math-d geo-c

Naomba msinishauri kwenda advance sihitaji kabisa imepoteza ndoto za wengi waliojiita madaktar mainjinia na ma pcb, pcm zao
 
System ya NACTE imefungwa jana Usiku labda usubiri hadi mwakani
 
Sawa. Ila huko chuoni unakotaka kwenda utakutana na hao madaktari watakufundisha wewe pamoja na wengine!! Sijui kama na wao wangeamua kuishia form 4 nakuwa na mawazo kama yako...nani angekuwafundisha hao mnaotaka kwenda diploma.
Jambo usilolijua au kama huna data za kutosha kuhusu suala fulani, ni bora ukanyamaza kwenye hili ("advance sihitaji kabisa imepoteza ndoto za wengi waliojiita madaktar mainjinia na ma pcb, pcm zao").
 
Je vyuo kama dit, atc inakuaje kwa indirectly
Vyuo vyote hvo vina select direct kupitia nacte omba Pre entry Dit usome wiki kumi na mbili then uanze ordinary diploma three years jiandae kujisomesha ada ina range 1 million bila accommodation wala Chakula Soma Electrical,Civil au Biomedical equipment
 
-matokeo yangu ni kama yafuatavyo physics-c Chem-c bios-c math-d geo-

basi nawe unajiona ndo umefaulu sanaaa masikini weee nafuu yule dogo alietimuliwa UDOM
 
-matokeo yangu ni kama yafuatavyo physics-c Chem-c bios-c math-d geo-

basi nawe unajiona ndo umefaulu sanaaa masikini weee nafuu yule dogo alietimuliwa UDOM
..

Broo unachoongea hauijui hivi GPA/Brn utafananisha division usiongee kwa kujifariji na sijaomba uncomment unajikuta mjuaji sana
 
..

Broo unachoongea hauijui hivi GPA/Brn utafananisha division usiongee kwa kujifariji na sijaomba uncomment unajikuta mjuaji sana
Alichomaanisha jamaa ni hata kama ingekua division bado chuo cha serikali huwezi Pata kumbuka kwenye vyuo vya serikali competition inakua kubwa sababu Kuna na form six walio temwa degree ya medicine that's why with those CCC I guarantee chuo cha serikali sahau,....
 
Back
Top Bottom